Monday, December 21, 2015

Upasuaji kwa njia ya Roboti




Hospitali moja katika manispaa ya Chongqing nchini China imefaulu kutumia roboti kufanya upasuaji wa kutoa uvimbe kutoka mwili wa mgonjwa wa saratani ya kongosho.Hospitali hiyo imesema kuwa huo ulikuwa upasuaji wa kwanza wa aina hiyo kuwahi fanywa na roboti kote duniani.


Thursday, December 17, 2015

Maelfu waandamana kupinga utawala wa Zuma


Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikuu ya Afrika Kusini wakitaka kutimuliwa kwa Rais Jacob Zuma kwa madai kuwa visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka sana.

Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika Kusini.
Zuma
Mwandishi wa BBC Karen Allen aliye nchini humo anasema

Video ya dk 4 ikimuonesha Balozi Ombeni Sefue akizungumzia kutenguliwa kwa Dr.Hosea TAKUKURU

SOURCE: MICHUZI BLOG

Wednesday, December 16, 2015

Magufuli amfuta mkuu wa kupambana na rushwa Dr.Edward Hosea



MagufuliIma














Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Rais Magufuli amesema hajaridhishwa "na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.”
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Dkt Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Kwa mujibu wa Bw Sefue, Dkt Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa "utendaji kazi wa Takukuru chini ya Dkt Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka”.
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takukuru ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
source: BBC swahili