Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka
miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya
kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi
katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa
katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita
2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.

Mwenyekiti
wa stand united Amani Vicent (kushoto) akibadilishana mkataba wa
udhamini wa timu hiyo na Makamu wa rais wa ACACIA anaeshugulikia masuala
ya Kampuni, Deo Mwanyika mara baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka
miwili na kampuni hiyo.
Udhamini
wa ACACIA katika misimu hii miwili ya ligi kuu itasaidia katika kuifanya
timu ya Stand United iweze kufanya vizuri katika michezo yake, pamoja
na kusaidia katika kuboresha programu mbalimbali za timu na kuendeleza
vipaji pamoja na masuala ya Utawala.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo Makamu wa rais wa Acacia aneshughulikia masuala ya
kampuni, Deo Mwanyika, amesema “Kwa takriban mwaka mmoja, tumekua
tukifanya kazi pamoja na Stand United. Kwa muda huo tulianzisha mchakato
wa kutambua namna nzuri ya kuboresha ushirikiano wetu ili kunufaisha
watu wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bwana Deo
amesema Msimu uliopita uliwapatia fursa nzuri ya kushuhudia uwezo wa
timu hiyo hasa ukizingatia ilikua mara yao ya kwanza kushiriki ligi kuu,
“Baada ya tathmini ya kina, tunadhani huu ni muda muafaka wa sisi
kusaini makubaliano au mkataba wa kuidhamini na kufanya kazi pamoja ya
kuikuza timu hii ya nyumbani maarufu kama “Chama la wana”.

Baadhi ya wachezaji wa Stend United
wakiwa na baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi
unaomilikiwa na kampuni ya Acacia ambao ni wadhamini wa timu hiyo muda
mfupi mara baada ya kuzindua rasmi jezi za timu hiyo zitakazotumika
katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza tarehe
12.09.2015
Hivyo,
Leo, Acacia tunasaini mkataba na timu ya Stand United kwa udhamini wa
misimu miwili ya ligi kuu, wenye thamani ya Shilingi bilioni moja.
Udhamini huu unajuamuisha shughuli za uendeshaji wa timu, kuboresha
uongozi na kukuza vipaji.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent, amesema udhamini
huo wa miaka miwili utakuwa chachu kwa timu yake kufanya vizuri katika
ligi kuu, “Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi ya nane na kipindi
hicho hatukuwa na fedha ya kutosha kuendesha timu, lakini kwa udhamini
tulioupata kutoka kwa ndugu zetu wa Acacia vijana wetu safari hii
watafanya vizuri zaidi.
Kampuni
ya Acacia ni kampuni inayoongoza kwa shughuli za uchimbaji wa madini
hapa Tanzania huku ikiwa na Migodi mitatu katika kanda ya ziwa, kupitia
mradi wa “Acacia Maendeleo Fund” ambao ndio pia umetoa udhamini wa timu
ya Stend umekuwa pia ukitekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa
Jamii hapa nchi huku kampuni hiyo ikieleza kuwa dhamira yake ni
kuendelea kufanya kazi na Jamii zinazowazunguka katika kuwaletea
Maendeleo wenyeji.
SOURCE: Mjengwa blog
0 comments:
Post a Comment