Wednesday, July 9, 2014

Huyu ndiye mfungaji mwenye magoli mengi zaidi katika historia ya fainali za Kombe la Dunia "Mjerumani, "Miroslav Klose" Avunja rekodi ya Ronaldo De Lima wa Brazil

Miroslav Klose amevunja rekodi ya Ronaldo na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya fainali za kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia  na kufikisha mabao 16.
Lilikuwa bao lake la pili katika mashindano baada ya kufunga bao akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Ghana,  hatua ya makundi na kumfanya alingane mabao na gwiji wa Brazil. Wafungaji waliofunga magoli mengi zaidi katika mashindano ya kombe la dunia muda wote ni pamoja na Miroslav Klose 16, Ronaldo De Lima 15 , Gerd Muller 14,  Just Fontaine 13,  Pele 12, Jurgen Klinsmann 11, Gary Lineker 10.
Klose alicheza kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia mwaka 2002 na kufunga mabao matatu `hat-trick` katika ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya  Saudi Arabia. 
Alifunga tena bao katika mechi iliyofuata ya makundi ambayo Ujerumani ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri ya  Ireland, kabla ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Cameroon.
Licha ya Ujerumani kufika fainali mwaka ule, Klose alishindwa kufunga tena katika mashindano, akimaliza michuano kwa idadi sawa ya mabao na Rivaldo, nyuma ya mfungaji bora, Ronaldo aliyefunga mabao 8.
Miaka minne baadaye, Ujerumani walikuwa wenyeji wa fainali za dunia (2006), mshambuliaji huyo alifunga mabao matano tena ambayo yalitosha kumpatia kiatu cha dhahabu.
Alifunga mabao mawili katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Costa Rica ambao walishinda mabao 4-2, alifunga mengine mawili katika mchezo wao wa mwisho wa makundi dhidi ya Ecuador.
Klose bao lake la mwisho katika fainali za kombe la dunia mwaka huu lilikuwa katika dakika ya 80. Bao la kusawazisha dhidi ya Argentina kwenye mchezo wa robo fainali na kufanya matokeo yawe 1-1, na Ujerumani wakashinda kwa mikwaju ya penati.
Na mwaka 2010, alifanikiwa kufunga mabao mengine manne: moja kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Australia, lingine katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya England hatua ya makundi na mawili katika ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Argentina hatua ya robo fainali. Kwa hisani ya #Shafii Dauda#

0 comments:

Post a Comment