Monday, July 14, 2014

Mario Gotze apeleka furaha iliyokosekana Ujerumani takribani miaka 24


Na Fredrick Majula
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Buyern Munich Mario Gotze ameibuka shujaa wa taifa la Ujerumani baada ya kuipatia timu yake ya taifa ubingwa wa dunia kwa goli pekee alilofunga dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali uliyofanyika katika uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro nchini Brazil. Gotze aliyeingia kuchukua nafasi ya mkongwe Miloslav Klose katika dakika ya 88 aliweza kufunga goli hilo muhimu mnamo dakika ya 113 katika muda wa nyongeza wa dk 30 baada ya kutoshana nguvu katika dk 90. 

Wednesday, July 9, 2014

Huyu ndiye mfungaji mwenye magoli mengi zaidi katika historia ya fainali za Kombe la Dunia "Mjerumani, "Miroslav Klose" Avunja rekodi ya Ronaldo De Lima wa Brazil

Miroslav Klose amevunja rekodi ya Ronaldo na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya fainali za kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia  na kufikisha mabao 16.
Lilikuwa bao lake la pili katika mashindano baada ya kufunga bao akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Ghana,  hatua ya makundi na kumfanya alingane mabao na gwiji wa Brazil. Wafungaji waliofunga magoli mengi zaidi katika mashindano ya kombe la dunia muda wote ni pamoja na Miroslav Klose 16, Ronaldo De Lima 15 , Gerd Muller 14,  Just Fontaine 13,  Pele 12, Jurgen Klinsmann 11, Gary Lineker 10.
Klose alicheza kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia mwaka 2002 na kufunga mabao matatu `hat-trick` katika ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya  Saudi Arabia. 
Alifunga tena bao katika mechi iliyofuata ya makundi ambayo Ujerumani ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri ya  Ireland, kabla ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Cameroon.
Licha ya Ujerumani kufika fainali mwaka ule, Klose alishindwa kufunga tena katika mashindano, akimaliza michuano kwa idadi sawa ya mabao na Rivaldo, nyuma ya mfungaji bora, Ronaldo aliyefunga mabao 8.

Hiki ndicho alichokisema Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari baada ya kipigo cha 7-1 toka kwa Wajerumani




Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
Lilikuwa chaguo langu. Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango chetu cha mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani. Hatukukata tamaa na kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya kufungwa bao la kwanza na kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani hawawezi kuelezea ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa kuheshimu hilo.
Tunatakiwa kujifunza jinsi ya kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu wa Brazil ni huu. Tafadhali watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi kwasababu hatujaweza kufika fainali-na tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi ya tatu. Bado tuna sababu ya kucheza.”