
Na Fredrick Majula
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Buyern Munich Mario Gotze ameibuka shujaa wa taifa la Ujerumani baada ya kuipatia timu yake ya taifa ubingwa wa dunia kwa goli pekee alilofunga dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali uliyofanyika katika uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro nchini Brazil. Gotze aliyeingia kuchukua nafasi ya mkongwe Miloslav Klose katika dakika ya 88 aliweza kufunga goli hilo muhimu mnamo dakika ya 113 katika muda wa nyongeza wa dk 30 baada ya kutoshana nguvu katika dk 90.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alipokea pasi kutoka kwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Andre Schurrle ambapo aliutuliza kifuani mpira huo na kuujaza nyavuni hivyo kuandika historia ya pekee katika maisha yake ya soka.

Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Ujerumani ilishinda Kombe hilo mwaka 1954, kisha 1974 na 1990, wakati huo bado ikiwa imegawika kati ya mashariki na magharibi. Ushindi wa mwaka huu ni wa kwanza tangu mashariki na magharibi kurudi tena kuwa taifa moja la Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment