Wednesday, May 25, 2016

Bill Cosby atakiwa mahakani



Image copyrightREUTERS
Jaji nchini Marekani ameamuaru mchekeshaji, Bill Cosby, kusimama mahakamani dhidi ya kesi kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia.
Cosby anatuhumiwa kwa makosa ya kumdhalilisha wanawake katika makazi yake mnamo mwaka 2004 baada ya kumlewesha kwa kitu kinachodaiwa dawa za kulevya.
Mchekeshaji huyo,ambaye awali kabla ya masahibu haya alikuwa ni mmoja miongoni mwa wachekeshaji maarufu wa runinga nchini Marekani, tayari amekwisha kumbana na misukosuko ya kukabiliwa na wimbi la madai unyanyasaji wa kijinsia.
Wanawake waliowengi, ambao alikuwa na mahusiano nao miaka ya 1960 wao hawawezi tena kufungua mashtaka ya jinai. Kufuatia hali hiyo Cosby amekana madai yote yanayomkabili.
Source:BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment