Thursday, May 26, 2016

Profesa Jay azungumza kwa mara nyingine Bungeni

 Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa siku ya pili mfululizo imeendelea kujadiliwa tangu ilivyoombwa na Waziri Jumanne Maghembe kiasi cha Sh. 135,797,787,000 .
Wabunge mbalimbali walipata nafasi ya kuchangia maoni yao, nakukutanisha na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa Jay aliposimama na kusema…>>>
Kama kweli tunataka tulinde rasilimali zetu na wanyama wetu tuwape wananchi elimu ili wajue vitu vya kufanya na vipi si vyakufanya, lakini sasa hivi ndugu zetu wanaokaa karibu na mbuga wameonekana kuwa wanateswa.
‘Na niwaambietu Mikumi kuna watu wengine tumezika nguo kwasababu hata maiti zao hatukuweza kuzipata kwasababu wamepigwa risasi ndani ya hifadhi. Kwa hiyo kutokana na hilo tunataka tuisisitize Serikali kama kweli mnataka tulinde rasilimali za Mikumi’
Tupunguze uadui huu kati ya Wananchi wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana kwenye hifadhi  na watu wa hifadhi. Tunapaza sauti ndugu zetu wanakufa lakini hakuna linalochukuliwa lolote
Full video ya Profesa Jay nimekuwekea hapa chini, ukimaliza kuitazama niachie maoni yako ili akipita baadae azisome

0 comments:

Post a Comment