Sunday, May 22, 2016

Hii ndiyo Meli Mpya Kubwa Duniani, Inachukua Abiria 6,780


Mapema wiki hii meli ambayo ina uwezo wa kuchukua abiria 6,780 iling’oa nanga Southampton kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya uzinduzi rasmi, Watu 3000 wamepata bahati kupanda  meli hii kubwa duniani. Meli hiyo inayojulikana kwa jina la Harmony of the sea ilitoka Southampton siku ya jumapili katika safari yake ya kwanza ya kibiashara kabla haijarudi tena Uingereza.
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha muonekano wa Meli hiyo
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
KKKKKKK
.
.
.
.
male
.
Source: Millard ayo

Monday, May 16, 2016

Aliyesababisha Mandela akamatwe akiri



Image copyrightB
Image captionMandela alikamatwa mwaka 1962 saa za usiku karibu na mji wa Durban.

Ajenti mmoja wa zamani wa shirika la ujasusi la marekani CIA, amekiri kuwa ndiye aliwafahamisha polisi wa Afrika kusini aliko rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela, ambaye baadaye alikamatwa na kufungwa miaka 27 jela kwa kupinga utawala wa wazungu.
Ufichuzi huo uliofanywa na gazeti la Sunday Times muda mfupi kabla ya ya kifo cha jasusi mmarekani Donald Rickard, unafichua kuwa Mandela ambaye alikuja kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Afrika kusini alikuwa akifuatiliwa na CIA.

Image copyrightAFP
Image captionMandela alikuwa rais mweusi wa kwanza nchini Afrika Kusini.

Mandela alikamatwa mwaka 1962 saa za usiku karibu na mji wa Durban akijifanya kuwa dereva wa texi, wakati gari lake lilisimamishwa kwenye kizuizi cha polisi.
Sasa ufichuzi wa ajenti huyo wa zamani wa CIA marehemu Donald Rickard unathibitisha ramsi kuwa ni yeye aliwajulisha polisi hatua ambayo ilisababisha Mandela kuwa mfungwa maarufu zaidi duniani.

Image copyrightAFP
Image captionUfichuzi huo unatarajwa kuiwekea shinikizo CIA kuitaka kutoa habari kuhusu kukamatwa kwa Nelson Mandela.

Wakati huo kiongozi yeyote wa kundi lililojihami alitajwa kuwa gaidi na mkomisti hatari zaidi nje ya muungano wa usovieti na tisho kwa nchi za magharibi.
Hata hivyo Mandela alikana kuwa mwanachama wa chama cha kikomisti.
Ufichuzi huo unatarajwa kuiwekea shinikizo CIA kuitaka kutoa habari kuhusu kuhusika kwake katika kukamatwa kwa Nelson Mandela na uungaji mkono wake serikali ya ubaguzi wa rangi.
source:BBC Swahili

Friday, May 13, 2016

Riadha: WADA yataka Kenya ipigwe marufuku


Image copyright
Image caption

Kenya inakabiliwa na changamoto upya kuhusiana na sheria ya kukabili matumizi ya madawa ya kututumua misuli miongoni mwa wanariadha wake.
Licha ya nchi hiyo kupitisha sheria mwezi uliopita iliyowezesha kubuniwa kwa halmashauri ya kupigana dhidi ya madawa yaliyopigwa marufuku, kamati ya nidhamu ya shirikisho la kupambana na madawa yaliyopigwa marufuku duniani WADA inasisitiza kuwa sheria hiyo haikuafikiana na mapendekezo ya WADA.
Kamati hiyo inapendekeza kuwa hatua ichukuliwe dhidi ya Kenya kwa kujumuisha vipengee fulani ambavyo vinakinzana na kanuni za WADA.
BBC imebaini kuwa halmashauri kuu ya WADA itakubali mapendekezo hayo katika mkutano wao mkuu baadaye leo mjini Montreal Canada.
Iwapo hilo litatekelezwa basi itakuwa wajibu wa kamati ya olimpiki duniani IOC kuipiga marufuku Kenya kutoshiriki mashindano yake hadi pale itakapotekeleza masharti iliyowekewa.
WADA ilikuwa imeipa Kenya makataa mapya ya hadi Mei 2 kuidhinisha sheria hiyo la sivyo ikabiliwe na hatari ya kuadhibiwa.

Image copyrightEPA
Image captionTakriban wanariadha 40 wameadhibiwa na shirika la riadha duniani (IAAF) kwa kupatikana wakiwa wametumia dawa hizo tangu mwaka 2012.

Mswada huo mpya unaharamisha matumizi ya dawa za kusisimua misuli na kuweka mikakati ya kukabiliana na wanaohusika ilipitishwa na kuwa sheria na rais Uhuru Kenyatta.
Takriban wanariadha 40 wameadhibiwa na shirika la riadha duniani (IAAF) kwa kupatikana wakiwa wametumia dawa hizo tangu mwaka 2012.
Bingwa mtetezi wa mbio za Boston marathon na Chicago pia ni miongoni mwa walioadhibiwa.
WADA ilikuwa imetoa masharti makali ya kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwili, pamoja na kutolewa kwa ufadhili wa kila mwaka wa $50,000 milioni kwa idara ya kukabiliana na tatizo hilo.
Tatizo la dawa zilizoharamishwa Kenya

Image copyrightB
Image captionBingwa mtetezi wa mbio za Boston marathon na Chicago Ritah Jeptoo pia ni miongoni mwa walioadhibiwa.

Kufikia 2011, zaidi ya wanariadha 40 walikuwa wamepatikana wametumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Kufikia Januari 2016, wanariadha 18 wa Kenya walikuwa wanatumikia marufuku
Wanariadha hao 18 walikuwa wanatumikia marufuku ya jumla ya miaka 55
Aidha, Rita Jeptoo mshindi wa marathon za Boston na Chicago pamoja na Lilian Moraa Mariita wanatumikia marufuku ndefu ya zaidi – miaka minane.
source:BBC Swahili

Monday, December 21, 2015

Upasuaji kwa njia ya Roboti




Hospitali moja katika manispaa ya Chongqing nchini China imefaulu kutumia roboti kufanya upasuaji wa kutoa uvimbe kutoka mwili wa mgonjwa wa saratani ya kongosho.Hospitali hiyo imesema kuwa huo ulikuwa upasuaji wa kwanza wa aina hiyo kuwahi fanywa na roboti kote duniani.


Thursday, December 17, 2015

Maelfu waandamana kupinga utawala wa Zuma


Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikuu ya Afrika Kusini wakitaka kutimuliwa kwa Rais Jacob Zuma kwa madai kuwa visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka sana.

Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika Kusini.
Zuma
Mwandishi wa BBC Karen Allen aliye nchini humo anasema

Video ya dk 4 ikimuonesha Balozi Ombeni Sefue akizungumzia kutenguliwa kwa Dr.Hosea TAKUKURU

SOURCE: MICHUZI BLOG

Wednesday, December 16, 2015

Magufuli amfuta mkuu wa kupambana na rushwa Dr.Edward Hosea



MagufuliIma














Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Rais Magufuli amesema hajaridhishwa "na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.”
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Dkt Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Kwa mujibu wa Bw Sefue, Dkt Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa "utendaji kazi wa Takukuru chini ya Dkt Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka”.
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takukuru ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
source: BBC swahili