Friday, October 10, 2014

Hong kong bado hapakaliki

WANAFUNZI: MAANDAAMANO BADO HONG KONG

Waandamanaji Hong Kong
Serikali ya eneo la Hong Kong imeitisha mazungumzo maalumu na viongozi wa wanafunzi ambao wamekuwa wakiratibu maandamano yaliyodumu kwa wiki mbili hadi sasa.
Mkutano huo wa serikali ya eneo hilo na wanafunzi unatarajiwa kufanyika leo.waandamanaji hao wanapinga utawala wa Beijing kuwachagulia mgombea katika uchaguzi mkuu wa eneo hilo 2017.
Hata hivyo wanafunzi hao wamesisitiza kuwa wataendelea na mgomo huo pamoja na serikali hiyo kuhitaji mazungumzo na viongozi wao.
Waandamanaji hao kwa sasa wamekuwa wakiendelea na maandamano huku baadhi ya huduma mhimu na kazi zikidorola.BBC

England yang'ara kwa vibonde San Marino

YAISAMBARATISHA SAN MARINO 5-0
Timu ya England imefanikiwa kupata ushindi mara mbili katika michezo miwili ya kundi E ya kufuzu kucheza michuano ya bara la Ulaya ya mwaka 2016 baada ya kupata ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya San Marino.
England alianza kuvuna magoli kupitia kwa mlinzi wake Phil Jagielka aliyefunga katika dakika ya 24 kwa mpira wa kichwa kabla ya Wayne Rooney kuongeza bao la pili kwa njia ya penalti katika dakika ya 43 kutoka na madhambi ya mchezaji wa San Marino Andy Selva.
Naye mshambuliaji Danny Welbeck alifanikiwa kutumbukiza goli la tatu kwenye dakika ya 49. Goli hili lilitokana na mpira wa pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Arsenal ambaye aliingia kipindi cha pili Alex Oxlade-Chamberlain.
Andros Townsend aliiongezea timu yake ya England goli la nne kwa mkwaju wa mbali kabla ya Alessandro Della Valle kujifunga mwenyewe kutokana na kugongwa na mpira uliopigwa na Rooney.
Matokeo ya michezo mingine: Belarus 0: Ukaraine 2, Macedonia 3: Luxembourg 2, Slovakia 2: Spain 1, Lithuania 1:Estonia 0, Slovenia 1: Switzerland 0, Liechtenstein 0: Montenegro 0, Moldova 1:Austria 2, Sweden 1: Russia 1 BBC

Hivi ndio vichwa vya habari za magazeti ya leo October 10 2014




.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

T.shirt ya maneno ya Kiswahili aliyovaa Seneta wa Nairobi ''Sonko'' ikiwatusi ‘wazungu’ 

UH 2Mike Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni Seneta wa jiji la Nairobi.

Hiki ni kiasi cha fedha walizotumia Barcelona kuwaleta marafiki Neymar kwenye utambulisho wake
Screen Shot 2014-10-10 at 9.16.37 AM
Usajili wa kumleta Neymar Dos Santos katika klabu ya FC Barcelona uligubikwa na utata mkubwa na hatimaye ulimgharimu Sandro Rosel kazi yake ya urais katika klabu hiyo ya Catalunya.

Monday, July 14, 2014