Mchezaji mwenye rekodi
ya pekee : Hakuwahi kupewa kadi ya aina
yeyote katika maisha yake ya soka
Na Fredrick Majula
Kempesi alianza safari yake
ya soka la kujulikana katika klabu ya Instituto de Cordoba mwaka 1973 ambayo
aliichezea msimu mmoja tu na baadae kujiunga na klabu ya Rosario Central msimu
uliofuata ambayo aliichezea kwa misimu miwili kutoka 1974-76, na kuifungia
jumla ya magoli 100 ndani ya misimu miwili. Msimu wa 1976/77 nyota ya Kempes
iling’aa hadi nchini Hispania ambapo Klabu ya Valencia iliweza kumsaini
mshambuliaji huyo, ni hapo ambapo mafanikio yake katika ngazi klabu yalionekana
kwani aliweza kutwaa vikombe viwili vya ligi ya Hispania, vikombe viwili vya
Kombe la washindi barani ulaya pamoja na kikombe kimoja cha klabu bingwa barani
ulaya. Pia katika misimu miwili mfululizo
Kempesi aliibuka mfungaji bora wa ligi ya Hispania akiwa kafunga jumla
ya magoli 24 msimu wa 1976/77 na ule wa 1977/78 alifunga jumla ya magoli 28.
Mario Kempesi aliitwa kuchezea kikosi cha timu ya taifa ya
Argentina kwa mara ya kwanza mwaka 1973 akiwa na umri wa miaka 19 tu katika
mechi za kufuzu kombe la dunia la mwaka 1974. Katika kukitumikia kikosi chake
cha timu ya Taifa, Kempesi alifanikiwa kucheza michuano 3 ya kombe la dunia
ikiwemo ile ya 1974, 1978 na ile ya 1982. Katika fainali hizo tatu ni michuano
ya mwaka 1978 ndio ilimuweka Kempes pamoja na Argentina katika historia ya
kuitwa bingwa wa kombe la dunia baada ya kushinda mchezo wa fainali dhidi ya
Uholanzi kwa jumla ya magoli 3 kwa 2 ya Uholanzi huku Kempes akifunga
magoli mawili katika ushindi huo, na
kupoza kiu ya miaka mingi kwa Argentina, ambayo haikuwahi kutwaa ubingwa wa
kombe hilo tangu michuano hiyo ianze mwaka 1930.
Pia katika michuano Mario aliibuka mshindi wa kiatu cha dhahabu.
Katika Safari yake ya soka la kimataifa
Mario Kempesi ni mchezaji ambaye hakuwahi kuoneshwa kadi ya njano wala kutolewa
uwanjani kwa kadi nyekundu mpaka kustafu kwake soka mwaka 1996. Kwa sasa Mario
Kempes ni mchambuzi wa michezo katika kituo cha televisheni ESPN.
0 comments:
Post a Comment