Baada ya mchezo huo Messi alinukuliwa akisema kuwa  'wakati wa kudhihirisha ukweli umewadia' ambapo walipata ushindi wa 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Slovenia. 

Nyota huyo wa klabu ya Barcelona anaamini kuwa kikosi hicho chini ya kocha Alejandro Sabella, kimeweza kuwa na hali ya kujimini ukilinganiasha na miaka miwili iliyopita na kudai kuwa kikosi hicho kinakwenda kuwania taji hilo nchini Brazil.

Akizungumza baada ya mchezo huo Messi alisema kuwa 'nilitamani kutoka kwenye benchi niingie uwanjani, kikosi chetu ni imara na tumejijengea imani, hiki ndicho tulichokuwa tunakitegemea baada ya Alejandro kuchukua timu.

"Naweza kuona sasa, wote tuna shauku. Muda wa kudhihirisha ukweli umewadia, tunakwenda Brazili tukiwa na matumaini makubwa.
Timu ya taifa ya Argentina itatupa karata yake ya kwanza katika michuano ya kombe la dunia June 15,  dhidi ya Bosnia-Herzegovina.