Bikira ni kigezo muhimu katika kujiunga na jeshi la Polisi la nchi hiyo.
Serikali
ya Indonesia inaelezwa kuruhusu kuwafanyia wanawake wanaotaka kujiunga
na Jeshi la Polisi kipimo cha bikira ,shirika la Human rights Watch
limeeleza.
Shirika hilo uangalizi wa haki za binaadam liliwahoji
Polisi wanawake na wanaotaka kujiunga na Jeshi la polisi ambao tayari
wamepimwa katika miji sita ya nchini Indonesia,wawili kati yao
wamefanyiwa kipimo hicho mwaka huu.
Kipimo cha bikira kimeorodheshwa kuwa moja ya matakwa ya kuingia kwenye Jeshi, tovuti ya polisi imeeleza.
Wanawake waliofanyiwa kipimo hicho wamesema walipata maumivu na kujisikia kudhalilishwa.
Askari wa kike walishapeleka malalamiko kwa ngazi za juu za jeshi la Polisi bila mafanikio.
Afisa
wa juu wa Human Rights Watch,Nisha Varia amesema kipimo hicho ni
unyanyasaji na kinawadhalilisha wanawake, amewataka polisi mjini Jakarta
kufuta kipimo hicho na kukipiga marufuku nchi nzima.
Polisi nao wanasema kuwa hawafanyi kipimo hicho kwa sasa kwa kuwa wamepiga marufuku.
Hata
hivyo hakuna ushahidi wa kutosha kuwa Jeshi la Polisi limesitisha
kitendo hicho kwa kuwa katika tovuti yake eneo la kazi tangazo la tarehe
5 mwezi Novemba mwaka 2014 imeeleza kuwa wanawake wanaotaka kuwa polisi
wanapaswa kujaribiwa kama wana bikira,hivyo basi wanawake wanaotaka
kuwa askari wanapaswa kutunza bikira zao.Wanawake walioolewa hawapewi
nafasi hiyo.
Mashuhuda wanasema kuwa jaribio la bikira hufanywa
katika hospitali zinazoendeshwa na jeshi la Polisi, vidole hutumika
katika kubaini kama mwanamke ni bikira au la.
Shirika la Human Rights Watch limesema kipimo hiki hufanywa na Polisi pia nchini Misri, India na Afghanistan.
Mwaka
2010 Brigedia Jenerali, Sigit Sudarmanto alieleza namna
alivyotofautiana na wenzake kuhusu kipimo cha bikira kwa wanawake yeye
haungi mkono.
Kisa cha kufanywa kwa kipimo hiki dhidi ya wanawake ni madai kuwa hawahitaji wanawake wasio bikira wakiwafananisha na makahaba.
Lakini
swali linabaki kuwa je kuna ushahidi wa kisayansi kuwa aliye bikira
hufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko asiye bikira, je asiye na bikira
hana adabu kuliko aliye nayo?
Sudarmanto amesema baada ya
kulumbana kwa muda mrefu iliridhiwa kusitishwa kwa zoezi hilo, hata
hivyo inashangaza kuona bado hali ni ileile japo ahadi ya kusitishwa
ilitolewa
0 comments:
Post a Comment