Wednesday, January 28, 2015

Kombe la mataifa ya Afrika 2015

Kundi D 
 
Cameroon vs Cote d'voire 

Guinea vs Mali

Kisa Cha Marafiki Watatu: Julius, Oscar Na Rashid..


 Ndugu zangu,

Nimeandika huko nyuma, kuwa watatu hawa, Julius Nyerere, Oscar Kambona na Rashid Kawawa, kuwa ndio walikuwa Watanganyika wenye nguvu na ushawishi mkubwa kwenye Tanganyika Huru.
Nchi ilikuwa changa, na viongozi nao walikuwa wachanga sana. Nyerere alikuwa mbele yake na dhamana kubwa aliyoibeba.
 

Nchi ilihitaji kujitambua, kisha kusonga mbele. Nyerere, mwalimu wa kawaida, ambaye hakupata hata kuwa Headmaster pale Pugu Sekondari, anaambiwa, kuwa sasa wewe ni Head Of State - Mkuu Wa Nchi.

Na wakati huo Dunia ilikuwa kwenye Vita Baridi. Iligawinyika kati ya Ubepari na Ukomunisti. Nyerere haliona, kuwa hatuwezi kuwa nchi ya kibepari, lakini, hatuwezi pia kuwa nchi ya Kikomunisti. Nyerere alialikwa Marekani, akafika China pia. Kuna mazuri aliyaona Marekani, na mazuri aliyaona China.

Sunday, January 18, 2015

JE UGUNDUZI WA KIFAA HIKI UTAWEZA KUPUNGUZA MICHEPUKO KATIKA MAHUSIANO?


Waswahili husema kwamba siku za mwizi ni arobaini. Msemo huo sasa huenda ukafanikishwa miongoni mwa akina baba ambao huenda kinyume na ndoa zao na wabakaji.

Hii ni baada ya kubuniwa kwa kifaa kwa jina Semenspy kilicho na uwezo wa kubaini majimaji yaliosalia katika chupi,nguo za kulalia,katika nguo na maeneo mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.

Kulingana na gazeti la the Nairobian nchini kenya,kifaa hicho pia kina mwongozo unaofanya mambo kuwa rahisi kwa wanandoa walio na shauku miongoni mwao.
Maagizo yake ni kwamba iwapo unamshuku mumeo ama mkeo tafuta majimaji hayo katika chupi ama nguo zilizotajwa hapo awali.

Kama kifaa cha kupima iwapo mwanamke ni mja mzito Semenspy kinaweza kubaini mara moja iwapo mtu ana uhusiano mwengine nje. Kulingana na daktari Wachira wa DIY Solutions, kifaa hicho kimetengezwa Marekani.Wachira amebaini kwamba amefanikiwa kupata majibu sahihi kutoka kwa wanawake wanaotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume wanawadanganya katika uhusiano.

Si rahisi kuwakamata wapenzi wanaodanganya kwa kuwa kunahitaji upelelezi zaidi na subra.
kwa kuwa kuna maji maji ya mbegu za kiume katika chupi ya mwanamume sio ushahidi kwamba mwanamume huyo anakwenda nje ya ndoa.

Swali ni vile utakavyoonyesha ushahidi kwamba maji maji hayo yanatoka kwa mwanamume huyo kwa kuwa mara nyingi wengi hutoa maji hayo bila ya kuhusika katika tendo la ngono. Daktari Wachira ana shauri kwamba mwanamke anayemchunguza mumewe anafaa kukaa kwa mda bila kufanya mapenzi, ili kuweza kuchukua sampuli za maji maji hayo kutoka kwa nguo za mumewe ama mpenziwe.

Ameongeza kuwa, violezi hivyo vinafaa kuchukuliwa mara tatu na kutoka nguo tofauti za mpenzi anayeshukiwa. Aidha si kila mara kwamba maji maji ya mbegu za kiume humtoka mwanamume bila ya kufanya mapenzi kwa hivyo hiyo haifai kuwa sababu ya mwanamume kujilinda.
SOURCE: BBC 

TANGAZO LA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2015


http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2014/09/Dr-Charles-Msonde.jpg

 Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania Dr. Charles Msonde

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015. 

Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT).

Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).

Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number).

Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. 

Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. 

Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015.