Hii ni baada
ya kubuniwa kwa kifaa kwa jina Semenspy kilicho na uwezo wa kubaini
majimaji yaliosalia katika chupi,nguo za kulalia,katika nguo na maeneo
mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.
Kulingana na
gazeti la the Nairobian nchini kenya,kifaa hicho pia kina mwongozo
unaofanya mambo kuwa rahisi kwa wanandoa walio na shauku miongoni mwao.
Maagizo yake ni kwamba iwapo unamshuku mumeo ama mkeo tafuta majimaji hayo katika chupi ama nguo zilizotajwa hapo awali.
Kama kifaa cha kupima iwapo mwanamke ni mja mzito Semenspy kinaweza kubaini mara moja iwapo mtu ana uhusiano mwengine nje. Kulingana
na daktari Wachira wa DIY Solutions, kifaa hicho kimetengezwa
Marekani.Wachira amebaini kwamba amefanikiwa kupata majibu sahihi kutoka
kwa wanawake wanaotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume
wanawadanganya katika uhusiano.
Si rahisi kuwakamata wapenzi wanaodanganya kwa kuwa kunahitaji upelelezi zaidi na subra.
kwa kuwa kuna maji maji ya mbegu za kiume katika chupi ya mwanamume sio ushahidi kwamba mwanamume huyo anakwenda nje ya ndoa.
Swali
ni vile utakavyoonyesha ushahidi kwamba maji maji hayo yanatoka kwa
mwanamume huyo kwa kuwa mara nyingi wengi hutoa maji hayo bila ya
kuhusika katika tendo la ngono. Daktari Wachira ana shauri kwamba
mwanamke anayemchunguza mumewe anafaa kukaa kwa mda bila kufanya
mapenzi, ili kuweza kuchukua sampuli za maji maji hayo kutoka kwa nguo
za mumewe ama mpenziwe.
Ameongeza kuwa, violezi hivyo vinafaa kuchukuliwa mara tatu na kutoka nguo tofauti za mpenzi anayeshukiwa. Aidha si kila mara kwamba maji maji ya mbegu za kiume humtoka
mwanamume bila ya kufanya mapenzi kwa hivyo hiyo haifai kuwa sababu ya
mwanamume kujilinda.
SOURCE: BBC
0 comments:
Post a Comment