Wednesday, November 25, 2015

Kama wewe unatafuta ajira, taarifa hii kutoka Secretariate ya Ajira na Utumishi wa Umma Tanzania Inakuhusu

Maelekezo muhimu ya ujazaji wa Taarifa kwenye mfumo wa Recruitment Portal kwa waombaji kazi


 Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa Umma imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa utumaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) ambao humsaidia muombaji kazi kutuma maombi hayo popote alipo ndani na nje ya Nchi kwa njia ya mtandao.
Ni muhimu kuzingatia kuwa kabla ya ujazaji wa taarifa kwenye mfumo wa ajira kila muombaji kazi lazima awe na barua pepe ambayo ni hai(Active email address) ambayo atatakiwa kujisajili katika sehemu iliyoandikwa Register katika ukurasa wa mbele wa mfumo (Home page) kabla ya muombaji kujaza taarifa zake katika vipengele 11 vilivyoelezewa kwenye makala haya. Pia kwa waombaji wote wanatakiwa kuhakikisha taarifa zao zote wanazojaza ni za uhakika na zipo katika ukamilifu.
 
Mfumo huu unapatikana kupitia anuani ya portal.ajira.go.tz ambapo baada ya usajili mwombaji kazi atajaza taarifa zake. Mgawanyo wa taarifa hizo upo katika vipengele vikuu 11 ambavyo ni Taarifa binafsi (Personal Details), Taarifa za Mawasiliano (Contact Details), Sifa za kielimu (Academic Qualifications), Sifa za Kitaaluma (Professional Qualifications), uwezo wa lugha (Language Proficiency), uzoefu wa kazi (Working Experience), Mafunzo, Warsha na Makongamano aliyowahi kuhudhuria (Training & Workshop Attended), ujuzi wa matumizi ya kompyuta (Computer Literacy), wadhamini (Referees), viambatanisho vingine (Other Attachments) na udhibitisho wa taarifa zilizoingizwa (Declaration). Aidha kila kipengele kinapaswa kujazwa kulingana na kinavyojieleza kwa ukamilifu wake.
Kwa kuwa kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya waombaji kazi kutojaza taarifa zao kikamilifu au kujaza baadhi ya taarifa zao kwenye vipengele visivyohusika, makala hii itajikita katika kuelezea kwa kina taarifa gani zinapaswa kujazwa kwa kila kipengele ili kuweka uelewa mpana kwa waombaji kazi kutokana na changamoto ambazo zimekua zikijitokeza kwa baadhi ya waombaji kazi kutozingatia masharti ya ujazaji wa taarifa hizo kikamilifu kwa kila kipengele kabla ya kutuma maombi ya kazi.  
Wapo baadhi ya waombaji kazi ambao wamekuwa wakijaza taarifa ambazo hazihusiani na kipengele husika hali inayoleta changamoto katika uchambuzi wa taarifa zao kwenye mfumo. Kwa kuzingatia changamoto hiyo na ili kukuza uelewa zaidi kwa waombaji kazi kupitia mfumo huo, yafuatayo ni maelezo muhimu yanayotakiwa kujazwa kwa kila kipengele kilichopo kwenye mfumo.

Tuesday, November 24, 2015

Pic of the Day

Mshindi wa ‪#‎AirtelTRACEMusicStar‬ @Mayungaa akiwa na @AKON 
nchini Marekani ambapo ameenda kwa ajiri ya kurekodi single moja 
na Star huyo wa Ghetto.

Mitandao ya Kijamii Kenya na Rais Magufuli wa Tanzania


Uchapakazi wa Rais Dkt John Magufuli unatuma ujumbe si kwa maafisa wa Tanzania pekee, bali na nchi za jirani pia na kuwaacha viongozi wa nchi hizo kwenye wakati mgumu. Kenya ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa kampeni, imeonesha kupenda mbinu za Magufuli na wananchi wake wanatamani mtu kama yeye.



Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Magufuli amefanya mambo makubwa na wananchi wamependa.
Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Muhimbili ilifichua uovu mwingi na kupelekea kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto. Ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali kwaajili ya kugharamia safari za nje za viongozi wa nchi, Magufuli aliamua kuzisitisha mara moja. Dkt Magufuli pia alielekeza kiasi cha shilingi milioni 225 zilichangwa kwaajili ya kugharamia hafla ya wabunge kupongezana mjini Dodoma 

zipelekwe kwenda kununua vitanda. Badala yake shilingi milioni 15 pekee zilitumika kwaajili ya sherehe hiyo.



Siku chache baadaye vitanda hivyo na vifaa vingine vilinunuliwa na kupelekwa Muhimbili. Jumatatu hii Magufuli alitangaza kuondoa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru 
December 9 na fedha za maandalizi hayo zitumike kwa mambo mengine muhimu. Hayo na mambo mengine yamefanya Dkt Magufuli atrend nchini Kenya. 

Hizi ni baadhi ya tweets za wakenya: