Sunday, October 12, 2014

Saudia yaamuru kuungwa mkono magaidi



Saudia yaamuru  kuungwa mkono magaidi
Wizara ya Mwongozo na Wakfu ya Saudi Arabia imewataka mahatibu misikitini  kuyaungwa mkono makundi ya kigaidi. Taarifa iliyotolewa leo na wizara hiyo imeeleza kuwa, makhatibu wa misikiti nchini humo wametakiwa watoe hutuba zinazounga mkono makundi ya kigaidi na yanayobeba silaha katika baadhi ya nchi za Kiislamu. Taarifa zinasema kuwa, misimamo hiyo ya Saudi Arabia ni mwendelezo wa sera za utawala wa Aal Saud za kuyaunga mkono makundi ya kitakfiri na kigaidi ambayo hadi sasa yamesababisha ghasia na machafuko katika baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati zikiwemo Syria, Iraq, Lebanon na Yemen. Imeelezwa kuwa, taasisi nyingi za kujitolea nchini Saudi Arabia ndizo zinazodhamini misaada ya kifedha kwa makundi ya kigaidi na kitakfiri yakiwemo Daesh, Jabhat Nusra na Taleban. 
IDHAA YA KISWAHILI YA TEHRAN

0 comments:

Post a Comment