Sunday, October 12, 2014

Sudan yawaibisha mabingwa wa Afrika


Wachezaji wa Nigeria
Mabingwa wateteza wa kombe la taifa bora barani Afrika Nigeria walishangazwa Ugenini baada ya kuchapwa bao moja kwa bila na Sudan na hivyobasi kusalia mkia katika kundi A la michuano ya kufuzu kwa faibnali za dimba hilo.
Bao la Bakri Almadina dakika chache tu kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika lilitosha kuiwezesha Sudan kushinda mchuano huo.
Kikosi cha Super Eagles chini ya Ukufunzi wa Stephen Keshi kilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili kuanzisha kampeni yake ya kufuzu,baada ya kushindwa na Congo Brazaville na kutoka sare na Afrika kusini .
Katika Matokeo ya mechi zengine:
Malawi 0-2 Algeria
Uganda 0-1 Togo
Ethiopia 0-2 Mali
Mozambique 2-0 Cape Verde
S Leone 0-0 Cameroon
Congo 0-2 South Africa
DR Congo 1-2 Ivory Coast
Niger 0-0 Zambia
Sudan 1-0 Nigeria
Gabon 2-0 B Faso
Guinea 1-1 Ghana

0 comments:

Post a Comment