Wataka pombe ionyeshe kiwango cha kalori kupunguza vitambi na unene wa kupitiliza
Pombe
inatakiwa kuwa na nembo inayoonyesha kiwango cha kalori au kipimo cha
joto litolewalo na chakula ili kupunguza vitambi au unene wa kupita
kiasi.
Madaktari wa afya ya umma, wameonya kuwa glasi kubwa ya
mvinyo inaweza kuwa na kiasi cha kalori 200- sawa na donati, aina ya
maandazi.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu hawajui madhara ya kula kiwango kikubwa cha kalori.
Waziri
wa Afya Jane Ellison amesema "hatua kubwa" imefanyika kwa kuviwekea
nembo vyakula, na kwa suala hilo serikali italiangalia.
Sekta ya
vinywaji imesema imesema iko tayari kwa wazo hilo la kuweka nembo zenye
kuonyesha kiasi cha kalori, lakini kuweka nembo zinazonyesha kiwango cha
kilevi katika kinywaji ni muhimu zaidi.
Uingereza ni moja ya
mataifa yenye watu wenye unene wa kupita kiasi duniani kwa kuwa na idadi
ya karibu robo ya watu wazima kuwekwa katika kundi la wenye unene wa
kupitiliza.
Vyakula tayari vinakuwa na taarifa za kiasi cha kalori
kilichomo ndani yake, lakini pombe haimo katika sheria za Umoja wa
Ulaya zinazotaka vyakula viwekewe nembo.Mvinyo nao watakiwa kuonyesha kiwango cha kalori
Na Tume ya Ulaya inaangaliwa iwapo vinywaji viwekewe nembo yenye kuonyesha kiasi cha kalori kilichomo.
Utafiti
uliofanywa na Chama cha Masuala ya Afya ya Jamii nchini Uingereza,
umesema hatua hii itaungwa mkono na wanywaji nchini Uingereza.
Mkuu
wa chama hicho cha RSPH, Shirley Cramer, ameiambia BBC: "Ni jambo la
kushtusha kweli - asilimia 80% ya watu wazima hawana wazo la kujua kiasi
cha kalori kilichomo katika kinywaji chochote na kama wanafikiri wana
wazo hilo kwa ujumla wanakadiria kiasi cha chini mno."
"Itasaidia taifa kupunguza watu wenye unene wa kupitiliza na huenda kupunguza kupunguza unywaji wa pombe."
Glasi
kubwa ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 8% ni kalori 170
Kiasi hicho hicho cha glasi ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia
14% ni kalori 230 Painti moja yenye asilimia 4% ya bia ni zaidi ya
kalori 180
0 comments:
Post a Comment