Sunday, April 26, 2015

Je,miraa inaongeza nguvu za kiume?



Wanaume katika eneo la Meru mashariki mwa Kenya ambao hawana uwezo wa kuwatosheleza wake zao kupitia tendo la ngono sasa wametakiwa kutokuwa na wasiwasi.
Mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo Florence kajuju ameanza mpango wa kuwahamasisha wanaume kutumia miraa badala ya ya pombe haramu .
Akizungumza na gazeti la The Nairobian nchini Kenya,kiongozi huyo amesema kuwa pombe haramu hushusha nguvu za kiume na kuwafanya wanaume kushindwa kuwatosheleza wake zao.
''Ni pombe kama hizi ambazo huathiri nguvu za kiume na kusababisha utasa miongoni mwa wanaume'',alisema.
Kajuju ambaye anasema anapenda miraa aliudhika alipogundua kwamba eneo la Meru ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaume hawana uwezo wa kutafuta watoto.
''Vijana wetu wameathirika vibaya na pombe haramu na lazima tuwaokoe''.
Alisema kuwa wale waliopiga marufuku uuzaji wa miraa katika mataifa yao wanafaa kugundua umuhimu wa zao hilo miongoni mwa jamii.
Source: BBC Swahili

Related Posts:

  • 13 Simple Tricks To A Long And Happy Marriage It's no secret that marriage takes work. After all, we're only human, and humans make mistakes, have bad days and sometimes even forget to load the dishwasher (again). Nevertheless, some couples are able to foster happy,… Read More
  • Stages of Surrender I have to confess that I used to suffer from a very significant disease. You might not have noticed it by looking at me, but if you had lived with me for awhile you probably would have. It has a very special name, and it’s … Read More
  • UN:Ebola kudhibitiwa kwa miezi mitatu David Nabarro Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ugonjwa wa Ebola David Nabarro ameiambia BBC kuwa mlipuko wa ugonjwa huo magharibi mwa Afrika unaweza kudhibitiwa katika kipindi cha miezi mitatu. Dr.Nabarro al… Read More
  • Hong kong bado hapakaliki WANAFUNZI: MAANDAAMANO BADO HONG KONG Waandamanaji Hong Kong Serikali ya eneo la Hong Kong imeitisha mazungumzo maalumu na viongozi wa wanafunzi ambao wamekuwa wakiratibu maandamano yaliyodumu kwa wiki mbili hadi sas… Read More
  • Sudan yawaibisha mabingwa wa Afrika Wachezaji wa Nigeria Mabingwa wateteza wa kombe la taifa bora barani Afrika Nigeria walishangazwa Ugenini baada ya kuchapwa bao moja kwa bila na Sudan na hivyobasi kusalia mkia katika kundi A la michuano ya kufuzu kwa faib… Read More

0 comments:

Post a Comment