Watawa katika mkutano na kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis
Idadi
ya wanawake wanaokuwa watawa imeongezeka pakubwa katika kipindi cha
miaka 25,kanisa katoliki nchini Uingereza na Wales limesema.
Takwimu
zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake wanaokula viapo vitakatifu
imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka mitano kutoka wanawake 15
mwaka 2009 hadi 45 mwaka uliopita,ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka
1990.
Wanawake 14 walioingia katika utawa mwaka 2014 walikuwa na miaka 30 ama chini yake ,takwimu mpya zinaonyesha.
Kanisa hilo linasema kuwa wanawake wanajiingiza katika maisha ya kidini kutokana na pengo la utamaduni kutotiwa maanani.
Takwimu
zinaonyesha kuwa mwaka 1980 takriban wanawake 80 walijiunga na utawa
lakini idadi hiyo ilipungua hadi mwaka 2004 ambapo wanawake saba pekee
walijiunga na utakatifu huo.
Idadi hiyo imeongezeka katika kipindi cha miaka 10 ambapo ilifika 45 mwaka 2014.
Watawa katika mkutano na kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis
0 comments:
Post a Comment