Monday, June 22, 2015

Jaji Warioba asema kitu juu ya wagombea urais CCM


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashangaa makada wanaojinadi kuwa ni wasafi na waadilifu, akisema sifa hizo zinatakiwa zitolewe na jamii.
Jaji Warioba, mmoja wa watu ambao wamekuwa wakikemea masuala ya ukiukwaji wa maadili, pia amesema hatamuunga mkono mgombea ambaye anakiuka maadili ya uongozi.
Tayari makada 37 wamejitokeza kuomba ridhaa ya wana-CCM kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wengi wao wamekuwa wakijinadi kuwa ni wasafi na waadilifu na kuwataka wanachama kutowapitisha watu wenye harufu ya ufisadi na wasio waadilifu.
Lakini Jaji Warioba alisema anaona wanakwenda kinyume na inavyotakiwa kufanyika.
“Viongozi wa sasa wanaonekana hawajali misingi ya maadili kwa sababu jamii yetu yenyewe imeonyesha kutochukizwa na suala hili la mmomonyoko wa maadili na wala jamii haijalipa uzito unaostahili,” alisema Jaji Warioba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Vuguvugu la uhuishaji wa Maadili kwa Jamii (Moral Rivival Movement).

Usher Raymond na Justin Beiber kulipa faini kwa kukopi wimbo wa "Somebody to Love"



Justin Bieber na Usher Raymond wamekutwa na shtaka na wametakiwa kulipa Dola million 10 baada ya kukopi wimbo "Somebody to Love" iliyofanyika mwaka 2010.

Muandishi wa nyimbo anayeafahamika kama Mareio Overton na muimbaji Devin Copeland anafahamika kama De Rico, wana wimbo wenye jina kama hilo hilo na wanawashtaki kwa wizi wa jina hilo (Copyrights Violation).
Wanasema ngoma hiyo inayo saini ya wakati sawa, beat, chords sawa na mashairi kwenye wimbo wao, Reuters imeripoti.
“Baada ya kusikiliza Copeland na wimbo wa Bieber na Usher, tuna hitimisha kwamba viitikio vyao vimefanana” Jaji Pamela Harris aliiandikia mahakama ya rufani.
Kesi hiyo ilifutwa Machi 2014 na Jaji wa U.S District ambae alihisi mahakama haiwezi kuona wizi wowote uliofanyika, Lakini Harris alisema kwamba mashairi “somebody to Love” imeimbwa “sawa kabisa na melody.
Source: Mjengwa Blog

Vilabu ruksa kusajili 7 wa kigeni Ligi Kuu Tanzania Bara




Kiwango cha ushindani Ligi kuu ya Tanzania Bara kinatarajiwa kuongezeka na kufungua milango zaidi kwa wachezaji wa kigeni baada ya vilabu kuruhusiwa kusajili wachezaji 7 wa kigeni kuanzia msimu ujao wa ligi.
Awali, baadhi ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara vilipendekeza usajili wa wachezaji 10 wa kigeni lakini Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) limeamua ni 7 tu wanaweza kusajiliwa na kucheza kwa wakati wote.
Katika misimu iliyopita, kila timu iliruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.
Hata hivyo, si vilabu vyote vitaweza kusajili wachezaji wa kigeni kwa kuwa na vyanzo vidogo vya pesa, bali vilabu vikubwa kama vile Simba,Yanga na Azam vitaweza kumudu gharama za usajili
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
- Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake kuanzia timu ya taifa au timu za vijana za U23, U20, U19 na U17.
- Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.
Wimbi la wachezaji wa kigeni linaongezeka nchini Tanzania baada ya ligi ya nchi hiyo kuwa ni ligi yenye ushindani na vilabu kutoa pesa nyingi kwa ajili ya usajili na mshahara.
Kwa habari zisizo rasmi, ligi ya Tanzania Bara inasemekana ndio ligi inayoongoza katika ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ushindani.
Source: BBC Swahili

Mchezaji wa kigeni kulipa Tanzania



Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limepitisha azimio la kila mchezaji wa kigeni kulipa dola 2,000 ( wastani wa milioni 5) kwa kila msimu atakaocheza ligi kuu ya Tanzania.
Kiasi hicho cha pesa kitaanza kulipwa katika msimu ujao wa ligi wa 2015/2016 .
Wachezaji wa kigeni waliosalia kuendelea kuchezea timu zao na wale wanaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao watalazimika kulipa kiasi hicho cha pesa.
Msemaji na afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilichoketi Jumamosi visiwani Zanzibar ni kuwa kiasi hicho cha pesa kitakuwa ni kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.
Katika miaka ya nyuma, wachezaji wa kigeni kutoka nchi mbalimbali, hasa za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walikuwa hawatozwi kiasi chochote cha pesa licha ya kulipwa mamilioni.
Kizuguto amesema fedha hizo zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu ujulikanao kama (Football Development Fund
Source: BBC Swahili