Tuesday, May 27, 2014

TETESI ZA USAJILI KATIKA MAGAZETI YA UINGEREZA LEO


meneja wa Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kumsajili beki wa Real Madrid Rafael Varane (Daily Mirror), Arsenal wapo tayari kutoa paundi milioni 3 kumwania nahodha wa Swansea, Ashley Williams (Metro), Arsenal pia wanamtaka kipa wa Cardiff David Marshall (Goal.com), inasemekana Rio Ferdinand anafikiria kwa makini hatua ya kujiunga na QPR baada ya kuondoka Man United (Guardian), boss wa Newcastle, Alan Pardew anataka kumsajili Steve Sidwell, Jack Colback, Wilfried Zaha na Ayoze Perez (Daily Star), Sunderland wameonesha nia ya kumsajili kipa wa Crystal Palace Julian Speroni (Daily Mail), Tottenham wamempa mkataba wa miaka mitatu meneja wa Southampton, Mauricio Pochettino, ambao anatarajiwa kusaini katika saa 48 zijazo (Daily Mirror).Source, Salim Kikeke.

0 comments:

Post a Comment