Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema mapema leo kuwa, uwazi na
uwajibikaji utasaidia kuharakisha maendeleo barani Afrika. Rais Kikwete
amesema hayo wakati wa kufungua rasmi mkutano wa takwimu huria barani
Afrika ulioanza leo jijini Dar es Salaam. Kwenye hotuba yake Rais
Kikwete amesema kuwa, serikali za Afrika zinapaswa kuweka wazi takwimu
zao ili raia wawe na ufahamu wa yale yanayofanywa na viongozi wao. Rais
wa Tanzania amesema kufanya hivyo kutaondoa misuguano inayoshuhudiwa
mara kwa mara kati ya raia na serikali hususan nyakati za matukio ya
kisiasa kama vile uchaguzi mkuu au kura ya maamuzi.
Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na zaidi ya wajumbe 400 kutoka
nchi kadhaa za Afrika wakiwemo wawakilishi wa serikali, sekta binafsi,
wataalamu na wasomi pamoja na wawekezaji.
SOURCE: TEHRAN
0 comments:
Post a Comment