Magaidi wa kundi la al Shabab wamedai kuchukua udhibiti wa miji
miwili kusini magharibi mwa Somalia siku chache tu baada ya kushambulia
kituo cha vikosi vya Umoja wa Afrika katika eneo hilo.
Msemaji wa al Shabab amesema kundi hilo limeteka miji miwili midogo
katika eneo la Lower Shabelle ambayo ni El Saliindi, yapata kilomita 65
kusini mwa Mogadishu na Kuntuwarey katika barabara ya Mogadishiu-Barawe.
Kaimu gavana wa Lower Shabelle, Ali Nur amethibitisha kuwa miji hiyo
miwili imeanguka mikononi mwa al Shabab. Aidha leo Jumamosi magaidi wa
kundi hilo la wakufurishaji wameshambulia msafara wa askari wa Umoja wa
Afrika katika mji wa Marka huko huko Lower Shabelle na kudai kuwa wameua
askari kadhaa. Septemba Mosi magaidi wa al Shabab walivamia kituo cha
askari wa Umoja wa Afrika huko Janale yapata kilomita 90 kusini mwa
Mogadishu na kuwaua askari 12 wa Uganda walio katika kikosi cha kulinda
amani cha Umoja wa Afrika.
SOURCE: Radio Tehran
0 comments:
Post a Comment