Tuesday, May 27, 2014

TETESI ZA USAJILI KATIKA MAGAZETI YA UINGEREZA LEO


meneja wa Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kumsajili beki wa Real Madrid Rafael Varane (Daily Mirror), Arsenal wapo tayari kutoa paundi milioni 3 kumwania nahodha wa Swansea, Ashley Williams (Metro), Arsenal pia wanamtaka kipa wa Cardiff David Marshall (Goal.com), inasemekana Rio Ferdinand anafikiria kwa makini hatua ya kujiunga na QPR baada ya kuondoka Man United (Guardian), boss wa Newcastle, Alan Pardew anataka kumsajili Steve Sidwell, Jack Colback, Wilfried Zaha na Ayoze Perez (Daily Star), Sunderland wameonesha nia ya kumsajili kipa wa Crystal Palace Julian Speroni (Daily Mail), Tottenham wamempa mkataba wa miaka mitatu meneja wa Southampton, Mauricio Pochettino, ambao anatarajiwa kusaini katika saa 48 zijazo (Daily Mirror).Source, Salim Kikeke.

Sunday, May 25, 2014

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA MCHEZO WA FAINALI KATI YA ATLETICO MADRID DHIDI YA REAL MADRID



Alex Livesey

Iker Casillas pamoja na Marcelo wakishangilia ushindi 


AFPAtletico Madrid's Brazilian-born forward Diego da Silva Costa (L) is substitutes by Atletico Madrid's forward Adrian Lopez during the UEFA Champions League Final.
 
Diego Costa akirudi katika bench dk 8 kipindi cha kwanza baada ya kushindwa kuendelea na mchezo


ReutersAtletico Madrid's Diego Godin (C) jumps and shoots the first goal for the team during their Champions League final
.
 
Goli la kwanza la Atletico Madrid lilitokana na mpira wa kichwa uliopigwa na beki wa timu hiyo Godin

HAYA NDIO MANENO ALIYOONGEA GARETH BALE BAADA YA KUTWAA TAJI LA KLABU BINGWA ULAYA




Kiungo mshambuliaji wa klabu ya real Madrid ya nchini Hispania Gareth Bale amekiri kuwa ilikuwa ni njozi yake kuisaidia klabu yake  kutwaa taji la kombe la ulaya( UEFA) baada ya kushinda ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya klabu ya Atletico Madrid katika muda wa nyongeza.

Tuesday, May 20, 2014

Tetesi za usajili Ulaya

Tetesi za soka kwenye magazeti ya Uingereza leo:
Liverpool na Inter Milan wanamtaka Ashley Cole (The Sun), Yaya Toure anataka kuondoka Manchester City kwa sababu hakuna mtu aliyemtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa wiki iliyopita (The Sun), Paris St-Germain wanataka kutoa pauni milioni 50 kumnunua Edin Hazard (Daily Mirror), Mario Mandzukic, huenda akajiunga na Manchester United baada ya kuzozana na Guardiola (Daily Mail), Man City wameanza mazungumzo ya kutaka kumsajili Bacary Sagna kutoka Arsenal (Daily Telegraph), Arsenal kumnyatia Serge Aurier, beki wa kulia kutoka Toulouse (Daily Star), Liverpool, Arsenal na Newcastle zinamtaka Mohamed Diame wa West Ham (Sun). source,Salim Kikeke

Barcelona yatangaza kocha Mpya


20140519-205430-75270957.jpg

*Barcelona wamteua Louis Enrique
Wakati Manchester United wakifanya uteuzi wa kocha, Barcelona nao waliopoteza taji msimu huu sawa na Man U wamemteua Luis Enrique kuwa kocha wa kikosi chao cha kwanza.

Taswira mbali mbali za taifa Stars dhidi ya Zimbabwe


IMG_0374
Bao pekee la John Bocco lililofungwa kipindi cha kwanza limeifanya Taifa Stars iibuke na ushindi katika mchezo wa kwanza kutafuta nafasi ya kuingia kwenye makundi ya kusaka nafasi ya kwenda Morocco mwakani katika kinyang’anyiro cha kombe la mataifa ya Africa.