Tuesday, May 20, 2014

Tetesi za usajili Ulaya

Tetesi za soka kwenye magazeti ya Uingereza leo:
Liverpool na Inter Milan wanamtaka Ashley Cole (The Sun), Yaya Toure anataka kuondoka Manchester City kwa sababu hakuna mtu aliyemtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa wiki iliyopita (The Sun), Paris St-Germain wanataka kutoa pauni milioni 50 kumnunua Edin Hazard (Daily Mirror), Mario Mandzukic, huenda akajiunga na Manchester United baada ya kuzozana na Guardiola (Daily Mail), Man City wameanza mazungumzo ya kutaka kumsajili Bacary Sagna kutoka Arsenal (Daily Telegraph), Arsenal kumnyatia Serge Aurier, beki wa kulia kutoka Toulouse (Daily Star), Liverpool, Arsenal na Newcastle zinamtaka Mohamed Diame wa West Ham (Sun). source,Salim Kikeke

0 comments:

Post a Comment