Sunday, May 25, 2014

HAYA NDIO MANENO ALIYOONGEA GARETH BALE BAADA YA KUTWAA TAJI LA KLABU BINGWA ULAYA




Kiungo mshambuliaji wa klabu ya real Madrid ya nchini Hispania Gareth Bale amekiri kuwa ilikuwa ni njozi yake kuisaidia klabu yake  kutwaa taji la kombe la ulaya( UEFA) baada ya kushinda ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya klabu ya Atletico Madrid katika muda wa nyongeza.


Akiongea na Skysports baada ya mchezo huo wa fainali, mchezaji huyo raia wa Wales aliyesajiliwa na real madrid  msimu uliopita akitokea klabu ya Tottenham ya nchini uingereza aliipatia goli la pili Madrid katika dakika ya 110 kwa mpira wa kichwa.

“Hiki ndicho mchezaji yeyote wa mpira wa miguu huota, kushinda taji la klabu bingwa ulaya, hakuna kitu kingine kikubwa katika ngazi ya kilabu kama taji hili.’’

“Ni hisia na furaha isiyoelezeka na itakuwa ni kumbukumbu milele. Kitu kikubwa kwangu ni kuwa tumecheza kama timu usiku wa leo na kutwaa taji ambalo ni la 10 kwa real Madrid.

Nimekuja Madrid kwa pesa, nimekuja kucheza katika mashindano makubwa na kushinda mataji kama tulivyofanya msimu huu.

Bale ambaye alikosa nafasi kadhaa kabla ya kuwafungia mabingwa hao goli muhimu ametoa pongenzi kwa Atletico Madrid ambao walinyakua ubingwa wa ligi ya Hispania mbele ya FC Barcelona na Real Madrid.

Aidha. katika mchezo huo beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Brazil Marcelo ndiye aliyeipatia Madrid bao la tatu kabla ya Cristiano Ronaldo kukamilisha ushindi huo kwa goli la nne alilolifunga kwa penalty na hivyo kuibuka mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kuweka rekodi ya kufunga jumla ya magoli 17.



0 comments:

Post a Comment