Tuesday, September 8, 2015

Kenya yaanzisha operesheni kuzima Alshabab

Rais Kenyatta amemuagiza inspekta mkuu wa polisi kuendesha operesheni dhidi ya ugaidi.


Operesheni hiyo inayoendeshwa na vikosi maalum vya kupambana na ugaidi kwa ushirikiano na jeshi la taifa linalenga wapiganaji takriban mia tatu wa Jeysh al Ayman wanaosadikika kujificha katika msitu huo. Kundi hilo la Jeysh al Ayman linasadikiwa kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Al Shabaab

Sunday, September 6, 2015

RAMSEY NOAH: Mimi na Siasa mbalimbali


Wakati wimbi la kisiasa likiwachukua wasanii wengi wa Tanzania kutoka tasnia ya muziki na wale wa maigizo( Bongo Movie), nchini Nigeria imekuwa tofauti kwa msanii wa maigizo nchini humo Ramsey Noah, ambaye pia ni staa wa movie ya Kibongo The Devil Kingdom aliyoshirikishwa na Marehemu Stevene Kanumba. Akizungumza na mtandao wa NET Nouah amekaririwa akisema kuwa

RAMSEYNOAHINTERVIEW
yuko tofauti kabisa na wasanii wenzake wa nchini humo wanaokimbilia kwenye siasa kila kukicha na kuongeza kuwa mashabiki wake wasitegemee Ramsey kujiunga na siasa.
Akifanyiwa mahojiano maalum na mtandao wa NET wa nchini humo, Ramsey alisema kuwa: ‘Sijui jinsi gani naweza kuwa mwanasiasa, mimi sio mwanadiplomasia kivile. Sijui namna ya kuyapangilia maneno yakafana kama wanasiasa wanavyoweza kufanya. Mimi siko hivyo’.
Source: NaijaGists.com

ACACIA Yaidhamini Stendi United kwa Kitita cha shilingi bilioni moja


Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita 2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.
 

Mwenyekiti wa stand united Amani Vicent (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini wa timu hiyo na Makamu wa rais wa ACACIA anaeshugulikia masuala ya Kampuni, Deo Mwanyika mara baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo.

Al Shabab wateka miji miwili kusini mwa Somalia

 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/fec01bb37336bdc554b56465a0fd13d5_XL.jpg
Magaidi wa kundi la al Shabab wamedai kuchukua udhibiti wa miji miwili kusini magharibi mwa Somalia siku chache tu baada ya kushambulia kituo cha vikosi vya Umoja wa Afrika katika eneo hilo.
Msemaji wa al Shabab amesema kundi hilo limeteka miji miwili midogo katika eneo la Lower Shabelle ambayo ni El Saliindi, yapata kilomita 65 kusini mwa Mogadishu na Kuntuwarey katika barabara ya Mogadishiu-Barawe.

Saturday, September 5, 2015

Hivi ndivo Juan Cuadrado alivofanyiwa na Shabiki wa Juventus kwa Mapenzi mema


Winga wa kimataifa wa Colombia na klabu ya Chelsea  Juan Cuadrado ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Juventus ya Italia, shabiki wake kafanya jambo hili la kuvutia baada ya kufurahishwa na ujio wa winga huyo katika klabu ya Juventus, hivyo kanyoa nywele kwa style ya picha ya Juan Cuadrado.
COAFg_rVEAI8OmS
Juan Cuadrado alijiunga na klabu ya Chelsea kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 27 pamoja na bonus akitokea klabu ya Fiorentina ya Italia ila amejiunga na Juventus kwa mkopo baada ya kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwa mabingwa hao wa Uingereza.
SOURCE: Millard ayo

MwanaHalisi yaachiwa Huru-

Toleo la gazeti la MwanaHALISI lililosababisha kufungiwa
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Diamond Platnumz atwaa Tuzo nchini Uganda


Kushoto ni tuzo aliyochukua Diamond Platnumz.
MKALI wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametwaa tuzo ya Msanii Bora wa Afrika katika tuzo zilizotolewa na Uganda Entertainment. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Diamond amewashukuru mashabiki wake waliompigia kura na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo pamoja na kuwaomba waendelee kumpigia kura katika vipengele vingine ambavyo anawania tuzo mbalimbali.

Diamond Platnumz.
Alichokiandika Diamond baada ya ushindi huo: SOURCE: Mjengwa blog


Mashehe 6 waliotekwa DRC wazungumza yaliyowasibu baada ya kurudi nchini


Ebola yatatiza tena Sierra Leone


Watu 1,000 nchini Sierra Leone wamewekwa kwenye karantini baada ya kugunduliwa kuwa mwanamke wa umri wa miaka 67 alifariki kutokana na Ebola.
Hilo limejiri siku tano tu baada ya kuanza kwa hesabu ya wiki sita iliyolenga kutangaza taifa hilo kuwa bila Ebola.

 Maafisa wa kukabili Ebola

Putin: Sera mbovu za Ulaya, sababu ya mgogoro wa wahajiri'


 
Rais Vladmir Putin wa Russia amesema leo kuwa, mgogoro wa wahajiri unaolikabili bara Ulaya kwa sasa umetokana na sera mbovu za kigeni za nchi za bara hilo hususan zile ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU). Kiongozi huyo amesisitiza kuwa, uingiliaji wa Wamagharibi katika mambo ya ndani nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni moja ya sababu za kuibuka mgogoro wa wahajiri katika nchi za EU.

Kikwete: Uwajibikaji utasaidia maendeleo ya Afrika

    kuzisha hati

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema mapema leo kuwa, uwazi na uwajibikaji utasaidia kuharakisha maendeleo barani Afrika. Rais Kikwete amesema hayo wakati wa kufungua rasmi mkutano wa takwimu huria barani Afrika ulioanza leo jijini Dar es Salaam. Kwenye hotuba yake Rais Kikwete amesema kuwa, serikali za Afrika zinapaswa kuweka wazi takwimu zao ili raia wawe na ufahamu wa yale yanayofanywa na viongozi wao. Rais wa Tanzania amesema kufanya hivyo kutaondoa misuguano inayoshuhudiwa mara kwa mara kati ya raia na serikali hususan nyakati za matukio ya kisiasa kama vile uchaguzi mkuu au kura ya maamuzi.
Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na zaidi ya wajumbe 400 kutoka nchi kadhaa za Afrika wakiwemo wawakilishi wa serikali, sekta binafsi, wataalamu na wasomi pamoja na wawekezaji.
SOURCE: TEHRAN