Rais wa
CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais mstaafu
Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo kikuu cha
Howard Washington, DC siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof
Venessa White Jackson.
Friday, April 24, 2015
Wanawake wanaokuwa watawa waongezeka UK kutoka 15 kwa mwaka hadi 45
By Unknown at 9:52:00 AM
No comments
Watawa katika mkutano na kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis
Idadi
ya wanawake wanaokuwa watawa imeongezeka pakubwa katika kipindi cha
miaka 25,kanisa katoliki nchini Uingereza na Wales limesema.
Takwimu
zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake wanaokula viapo vitakatifu
imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka mitano kutoka wanawake 15
mwaka 2009 hadi 45 mwaka uliopita,ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka
1990.
Boko Haram labadilisha jina Nigeria
By Unknown at 9:42:00 AM
No comments
Picha mpya zimetolewa kuhusu wapiganaji wa Boko Haram ambao wanajielezea kuwa Islamic State Jimbo la Magharibi mwa Afrika.
Wednesday, January 28, 2015
Kisa Cha Marafiki Watatu: Julius, Oscar Na Rashid..
By Unknown at 12:38:00 PM
No comments
Ndugu zangu,
Nimeandika
huko nyuma, kuwa watatu hawa, Julius Nyerere, Oscar Kambona na Rashid
Kawawa, kuwa ndio walikuwa Watanganyika wenye nguvu na ushawishi mkubwa
kwenye Tanganyika Huru.
Nchi ilikuwa changa, na viongozi nao walikuwa wachanga sana. Nyerere alikuwa mbele yake na dhamana kubwa aliyoibeba.

Nchi
ilihitaji kujitambua, kisha kusonga mbele. Nyerere, mwalimu wa kawaida,
ambaye hakupata hata kuwa Headmaster pale Pugu Sekondari, anaambiwa,
kuwa sasa wewe ni Head Of State - Mkuu Wa Nchi.
Na wakati huo Dunia ilikuwa kwenye Vita Baridi. Iligawinyika kati ya Ubepari na Ukomunisti. Nyerere haliona, kuwa hatuwezi kuwa nchi ya kibepari, lakini, hatuwezi pia kuwa nchi ya Kikomunisti. Nyerere alialikwa Marekani, akafika China pia. Kuna mazuri aliyaona Marekani, na mazuri aliyaona China.
Sunday, January 18, 2015
JE UGUNDUZI WA KIFAA HIKI UTAWEZA KUPUNGUZA MICHEPUKO KATIKA MAHUSIANO?
By Unknown at 4:30:00 PM
No comments
Hii ni baada
ya kubuniwa kwa kifaa kwa jina Semenspy kilicho na uwezo wa kubaini
majimaji yaliosalia katika chupi,nguo za kulalia,katika nguo na maeneo
mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.
Kulingana na
gazeti la the Nairobian nchini kenya,kifaa hicho pia kina mwongozo
unaofanya mambo kuwa rahisi kwa wanandoa walio na shauku miongoni mwao.
Maagizo yake ni kwamba iwapo unamshuku mumeo ama mkeo tafuta majimaji hayo katika chupi ama nguo zilizotajwa hapo awali.
Kama kifaa cha kupima iwapo mwanamke ni mja mzito Semenspy kinaweza kubaini mara moja iwapo mtu ana uhusiano mwengine nje. Kulingana
na daktari Wachira wa DIY Solutions, kifaa hicho kimetengezwa
Marekani.Wachira amebaini kwamba amefanikiwa kupata majibu sahihi kutoka
kwa wanawake wanaotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume
wanawadanganya katika uhusiano.
Si rahisi kuwakamata wapenzi wanaodanganya kwa kuwa kunahitaji upelelezi zaidi na subra.
kwa kuwa kuna maji maji ya mbegu za kiume katika chupi ya mwanamume sio ushahidi kwamba mwanamume huyo anakwenda nje ya ndoa.
Swali
ni vile utakavyoonyesha ushahidi kwamba maji maji hayo yanatoka kwa
mwanamume huyo kwa kuwa mara nyingi wengi hutoa maji hayo bila ya
kuhusika katika tendo la ngono. Daktari Wachira ana shauri kwamba
mwanamke anayemchunguza mumewe anafaa kukaa kwa mda bila kufanya
mapenzi, ili kuweza kuchukua sampuli za maji maji hayo kutoka kwa nguo
za mumewe ama mpenziwe.
Ameongeza kuwa, violezi hivyo vinafaa kuchukuliwa mara tatu na kutoka nguo tofauti za mpenzi anayeshukiwa. Aidha si kila mara kwamba maji maji ya mbegu za kiume humtoka
mwanamume bila ya kufanya mapenzi kwa hivyo hiyo haifai kuwa sababu ya
mwanamume kujilinda.
SOURCE: BBC
TANGAZO LA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2015
By Unknown at 4:19:00 PM
No comments
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania Dr. Charles Msonde
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu
wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT)
Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015.
Watahiniwa
watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015
hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa
wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa
wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT).
Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).
Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number).
Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).
Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number).
Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.
Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani.
Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015.