Chama cha
vilabu vikubwa vya soka barani ulaya (ECA) wanataka michuano ya kombe
la dunia ya mwaka 2022 yatayofanyika nchi Qatar yafanyike kati ya Mei 5
na Juni 4.
Shirikisho la soka duniani Fifa walitangaza mwezi uliopita kuwa michezo ya michuano hiyo itafanyika kati ya Januari na Februari au Novemba na desemba. Lakini mapendekezo yanayotolewa na Chama cha vilabu vikubwa vya soka (ECA) na wakilishi wa ligi za kulipwa ulaya (EPFL) wanataka mashindano hayo yacheze mwanzo mwa majira ya joto sababu itakua ndio salama kwa afya za wachezaji.
Uamuzi wa shirikisho la mpira dunia Fifa kuhusu wakati gani michuano hiyo ifanyike inatarajiwa kutolewa Machi mwaka 2015. ECA na
EPF wanaamini pendekezo yao mpya yanaonyesha jinsi mashindano inaweza
kuchezwa Mei na Juni bila kuhatarisha afya za wachezaji na viongozi.
Pia kufanyika kwa kombe la dunia mwezi mei na juni kutakua hakuna madhara kwa michuano ya klabu bigwa barani ulaya, michezo ya olimpiki na waumini wa dini ya kiislam watakua wamemaliza mfungo mtukufu wa Ramadhani
.Source: Mjengwa
0 comments:
Post a Comment