Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna anajiandaa kuanza kufanya kazi katika kampuni ya michezo Puma.Mwanamziki huyo ametangazwa kuwa mkurugenzi wa ubunifu wa vifaa vya kike na atakuwa uso wa vifaa vya mazoezi vya wanawake.
Rihana
mwenye umri wa miaka 26 ataunda aina ya nguo zilizopo pamoja na viatu
na kusaidia kubuni muundo mpya wa chapa cha bidhaa hizo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo,Rihana amesema anafurahi kuona ni nini yeye na Puma wanaweza kubuni.
Wakuu wa kampuni ya Puma wanasema kuwa Rihana ataleta ubunifu katika ulimwengu wa riadha.
Nguo
hizo mpya zitakuwa na mtindo wenye lengo la kuwaimarisha wanawake
katika mazoezi mbali na kuwafanya kuamini miili yao pamoja na wao
wenyewe. Jukumu la Rihana litakuwa kuwa na ushawishi katika bidhaa zitakazoundwa pamoja na kuandaa ukuzaji wa bidhaa mpya. Akiwa miongoni mwa kampeni ya Forever faster msanii huyo atashirikishwa na wanariadha kama viule Usain Bolt na Sergio Aguero.
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo Bjorn Gulden amesema kuwa waliamua kumtafuta mshirika
katika nguo za wanawake za kufanyia mazoezi kutokana na ushawishi mkubwa
wa kampuni hiyo katika soka,riadha na mashindano ya magari.Tunafurahi kumpata Rihana na tunajianda kuona ni nini tunaweza buni kwa ushirikiano wake.
Rihana si mtu wa kwanza nje ya michezo kujiunga na kampuni ya Puma. Msanii
50 cent na Jay Z walitoa viatu na kampuni ya Reebok, huku Kim
Kardashian akiwa uso wa viatu vya Sketchers na mumewe Kanye West
akifanya kazi na Nike pamoja na Adidas.
0 comments:
Post a Comment