Chama
cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa
Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile Super Mario
alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii. Adhabu hiyo
itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya
Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu
ya England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie kozi
ya elimu.
Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi. Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia, baada
ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook
kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa
"makosa".
Balotelli
aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema:
"nasikitika kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC
wataadhibiwa kwa kosa ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira
yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji
wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru
la FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.
"Hatua yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na mchezaji."
Mchezaji
huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya
mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa
Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya
sarafu kama myahudi."
Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.
Balotelli
alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United
katika uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita
kutokana na maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool
iliambulia kipigo cha magoli 3-0.
Balotelli ameifungia magoli
mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya Liverpool tangu
atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi.
Jaji Warioba asema kitu juu ya wagombea urais CCM
Dar es
Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba amewashangaa makada wanaojinadi kuwa ni wasafi na
waadilifu, akisema sifa hizo zinatakiwa zitolewe na jamii.
Jaji
Warioba, mmo…Read More
Kikwete: Uwajibikaji utasaidia maendeleo ya Afrika
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema mapema leo kuwa, uwazi na
uwajibikaji utasaidia kuharakisha maendeleo barani Afrika. Rais Kikwete
amesema hayo wakati wa kufungua rasmi mkutano wa takwimu h…Read More
Ebola yatatiza tena Sierra Leone
Watu 1,000 nchini
Sierra Leone wamewekwa kwenye karantini baada ya kugunduliwa kuwa
mwanamke wa umri wa miaka 67 alifariki kutokana na Ebola.
Hilo limejiri siku tano tu baada ya kuanza kwa hesabu ya wiki sita iliyolenga …Read More
0 comments:
Post a Comment