Thursday, December 18, 2014

Wabunge warushiana ngumi bungeni Kenya


Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
 
 Seneta Johnston Muthama alijikuta pabaya kwani suruali yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.


 
Seneta Muthama pia alijeruhiwa vibaya mguuni

Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.

Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia.

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Source: BBC

Related Posts:

  • Bill Cosby atakiwa mahakani Image copyrightREUTERS Jaji nchini Marekani ameamuaru mchekeshaji, Bill Cosby, kusimama mahakamani dhidi ya kesi kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia. Cosby anatuhumiwa kwa makosa ya kumdhalilisha wanawake katika makazi… Read More
  • Aliyesababisha Mandela akamatwe akiri Image copyrightBImage captionMandela alikamatwa mwaka 1962 saa za usiku karibu na mji wa Durban. Ajenti mmoja wa zamani wa shirika la ujasusi la marekani CIA, amekiri kuwa ndiye aliwafahamisha polisi wa Afrika kusini a… Read More
  • Kauli ya Louis van Gaal baada ya Ubingwa wa Kombe la FA kwa Man United Baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la FA akiwa na Man United, Louis van Gaalamezungumza kauli ya kujivunia, licha ya kuwa kibarua chake kipo mashakani kuchukuliwa na Jose Mourinho kwa… Read More
  • Upasuaji kwa njia ya Roboti Hospitali moja katika manispaa ya Chongqing nchini China imefaulu kutumia roboti kufanya upasuaji wa kutoa uvimbe kutoka mwili wa mgonjwa wa saratani ya kongosho.Hospitali hiyo imesema kuwa huo ulikuwa upasuaj… Read More
  • Hii ndiyo Meli Mpya Kubwa Duniani, Inachukua Abiria 6,780 Mapema wiki hii meli ambayo ina uwezo wa kuchukua abiria 6,780 iling’oa nanga Southampton kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya uzinduzi rasmi, Watu 3000 wamepata bahati kupanda  meli hii kubwa duniani. Mel… Read More

0 comments:

Post a Comment