Video
iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’itaanza
kuonyeshwa ijumaa ya leo December 19 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video
imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Video imetayarishwa
na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape
Town” .
Vituo vitakavyo rusha hii video
Cameroon, Ethiopia, Angola, U.S. & U.K. itachezwa kwenye vituo vya 1Musicnetworks.
Nigeria na Ghana itachezwa kwenye kituo cha SOUNDCITYtv.
Uganda itachezwa kwenye kituo cha NTV Uganda.
Kenya itachezwa kwenye kituo cha Citizen Tv kwenye kipindi cha Mseto.
Chama
cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa
Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile Super Mario
alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii. Adhabu hiyo
itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya
Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu
ya England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie kozi
ya elimu.
Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi. Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia, baada
ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook
kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa
"makosa".
Balotelli
aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema:
"nasikitika kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC
wataadhibiwa kwa kosa ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira
yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji
wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru
la FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.
"Hatua yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na mchezaji."
Mchezaji
huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya
mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa
Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya
sarafu kama myahudi."
Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.
Balotelli
alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United
katika uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita
kutokana na maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool
iliambulia kipigo cha magoli 3-0.
Balotelli ameifungia magoli
mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya Liverpool tangu
atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi.
Viongozi
wa Ulaya wamemaliza kikao chao mjini Brussels Ubelgiji, wakisema kwa
sasa wameungana zaidi kuliko ilivyokuwa awali katika kuikabili Urusi. Viongozi
hao wameonesha kuwa vikwazo vya kiuchumi havitadhoofishwa licha ya
matatizo ya kifedha yanayoikabili Urusi.
Badala yake hatua mpya za Umoja
wa Ulaya zilizokuwa zimewekwa kufuatia Urusi kulitwaa kimabavu jimbo la
Crimea zimepitishwa na zitaanza kutumika mwishoni mwa wiki hii.
Rais
mpya wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk akifunga kikao cha viongozi wa EU
amesema Urusi na vitendo vyake ni tatizo kubwa la kimkakati
linaloikabili Ulaya.
Akiongoza kikaocha wakuu wa nch ishirini na nane za Umoja
wa Ulaya. Bw. Tusk amesema kuwa vitendo vya Urusi ndani ya Ukraine na katika Ulaya ni
changamoto na alibaini kwamba mataifa ya Umoja wa Ulaya yameungana zaidi
kuliko ilivyowahi kuwa huko nyuma katika kukabiliana na Urusi.
Aidha, ameonya kuwa Ulaya inahitaji mkakati wa muda mrefu wa
aina yake,ambao si tu utakaoshughulikia matatizo katika wiki zijazo na
miezi, bali miaka. Wakati huo huo viongozi wamekubaliana vikwazo vipya
vinavyopiga marufuku uwekezaji katika jimbo la Crimea, ishara kwamba
vikwazo hivyo havitalegezwa hadi Urusi itakapobadili msimamo wake kuhusu
jimbo hilo.
“Mimi Nijiuzulu kwa sababu gani? yaani kwa sababu ya mafanikio ya
kuwakomboa wanawake kwenye Elimu ndio mimi nijuzulu,maana kujiuzulu
kunasababu, na hakuna sababu ya mimi kufanya hivyo na sitofanya hivyo
kwani wanaodai mimi nijiuzulu ni wanafiki wenye nia mbaya na mimi ,na
mimi sijiuzulu ng’o na nikifanya wanavyotaka Rais atashangaa ”alisema
Waziri Tibaijuka.
“Leo natuhumiwa na kila mtu kwamba nimepewa
pesa na Rugimalira kwamba ni za kifisadi,Jamani tuwe wa kweli kuhusu
madai haya maana nimepewa pesa na Rugemalira kwa ajiri ya shule hizi na
sio huyo pekee alliyechangia kwani waliochangia pesa hizi ni watu wengi
ikiwema Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Mfanya Biashara Maarufu
Reginald Mengi na wengine wengi,inakuwaje leo mchango wa Rugumarila kwa
Ajiri ya Elimu kwenye Shule hii ndio iwe nongwa”
“Kwasababu ukisema ni pesa alizonipa ni za ufisadi wa Escrow sio
kweli,kwani Bodi ya Shule ilimuomba Bwana Rugemalira pesa kwa kutumia
Kampuni yake ya Mabibo Wine na kipindi kile ndio alikuwa kiongozi, sasa
hawa watu wanaozani ni za ufisadi inakuwaje jamani tuwe
wakweli”Aliongeza Waziri Tibaijuka." Source:Clouds fm radio
Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna anajiandaa kuanza kufanya kazi katika kampuni ya michezo Puma.Mwanamziki huyo ametangazwa kuwa mkurugenzi wa ubunifu wa vifaa vya kike na atakuwa uso wa vifaa vya mazoezi vya wanawake.
Rihana
mwenye umri wa miaka 26 ataunda aina ya nguo zilizopo pamoja na viatu
na kusaidia kubuni muundo mpya wa chapa cha bidhaa hizo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo,Rihana amesema anafurahi kuona ni nini yeye na Puma wanaweza kubuni.
Wakuu wa kampuni ya Puma wanasema kuwa Rihana ataleta ubunifu katika ulimwengu wa riadha.
Nguo
hizo mpya zitakuwa na mtindo wenye lengo la kuwaimarisha wanawake
katika mazoezi mbali na kuwafanya kuamini miili yao pamoja na wao
wenyewe. Jukumu la Rihana litakuwa kuwa na ushawishi katika bidhaa zitakazoundwa pamoja na kuandaa ukuzaji wa bidhaa mpya. Akiwa miongoni mwa kampeni ya Forever faster msanii huyo atashirikishwa na wanariadha kama viule Usain Bolt na Sergio Aguero.
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo Bjorn Gulden amesema kuwa waliamua kumtafuta mshirika
katika nguo za wanawake za kufanyia mazoezi kutokana na ushawishi mkubwa
wa kampuni hiyo katika soka,riadha na mashindano ya magari.Tunafurahi kumpata Rihana na tunajianda kuona ni nini tunaweza buni kwa ushirikiano wake.
Rihana si mtu wa kwanza nje ya michezo kujiunga na kampuni ya Puma. Msanii
50 cent na Jay Z walitoa viatu na kampuni ya Reebok, huku Kim
Kardashian akiwa uso wa viatu vya Sketchers na mumewe Kanye West
akifanya kazi na Nike pamoja na Adidas.
Wabunge
wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku
wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama
ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge
lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili
mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao
maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye
utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Seneta Johnston Muthama alijikuta pabaya kwani suruali yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo
Mwenyekiti wa kamati ya usalama
wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko
yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na
kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.
Spika
wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa
baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa
kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao
umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi
nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa
kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Seneta Muthama pia alijeruhiwa vibaya mguuni
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia
ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa
faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha
ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa
kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab
wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia.
Rais
Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui
mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari
la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Chama cha
vilabu vikubwa vya soka barani ulaya (ECA) wanataka michuano ya kombe
la dunia ya mwaka 2022 yatayofanyika nchi Qatar yafanyike kati ya Mei 5
na Juni 4.
Shirikisho
la soka duniani Fifa walitangaza mwezi uliopita kuwa michezo ya
michuano hiyo itafanyika kati ya Januari na Februari au Novemba na
desemba. Lakini
mapendekezo yanayotolewa na Chama cha vilabu vikubwa vya soka (ECA) na
wakilishi wa ligi za kulipwa ulaya (EPFL) wanataka mashindano hayo
yacheze mwanzo mwa majira ya joto sababu itakua ndio salama kwa afya za
wachezaji.
Uamuzi wa shirikisho la mpira dunia Fifa kuhusu wakati gani michuano hiyo ifanyike inatarajiwa kutolewa Machi mwaka 2015.ECA na
EPF wanaamini pendekezo yao mpya yanaonyesha jinsi mashindano inaweza
kuchezwa Mei na Juni bila kuhatarisha afya za wachezaji na viongozi.
Pia
kufanyika kwa kombe la dunia mwezi mei na juni kutakua hakuna madhara
kwa michuano ya klabu bigwa barani ulaya, michezo ya olimpiki na waumini
wa dini ya kiislam watakua wamemaliza mfungo mtukufu wa Ramadhani