Friday, December 19, 2014

Video Ya AliKiba Kutoka Leo, Itarushwa Kwenye Vituo Hivi Kwa Mara Ya Kwanza

Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’itaanza kuonyeshwa ijumaa ya leo December 19 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Video imetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town” .

Vituo vitakavyo rusha hii video

Cameroon, Ethiopia, Angola, U.S. & U.K. itachezwa kwenye vituo vya 1Musicnetworks.

Nigeria na Ghana itachezwa kwenye kituo cha SOUNDCITYtv.

Uganda itachezwa kwenye kituo cha NTV Uganda.

Kenya itachezwa kwenye kituo cha Citizen Tv kwenye kipindi cha Mseto.

Tanzania itachezwa kwenye kituo cha CloudsTV.
SOURCE :Dj Fetty blog

Balotelli afungiwa mchezo mmoja na faini

Chama cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja, mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile Super Mario alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii. Adhabu hiyo itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu ya England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie kozi ya elimu.
 

Baloteli mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi. Balotelli amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia, baada ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa "makosa".

Balotelli aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema: "nasikitika kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC wataadhibiwa kwa kosa ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru la FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.

"Hatua yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na mchezaji."
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya sarafu kama myahudi."
Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.

Balotelli alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita kutokana na maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool iliambulia kipigo cha magoli 3-0.
Balotelli ameifungia magoli mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya Liverpool tangu atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi.
Source: BBC Swahili

Jumuiya ya Ulaya yaungana dhidi ya Russia



Viongozi wa Ulaya wamemaliza kikao chao mjini Brussels Ubelgiji, wakisema kwa sasa wameungana zaidi kuliko ilivyokuwa awali katika kuikabili Urusi. Viongozi hao wameonesha kuwa vikwazo vya kiuchumi havitadhoofishwa licha ya matatizo ya kifedha yanayoikabili Urusi.

Badala yake hatua mpya za Umoja wa Ulaya zilizokuwa zimewekwa kufuatia Urusi kulitwaa kimabavu jimbo la Crimea zimepitishwa na zitaanza kutumika mwishoni mwa wiki hii.

Rais mpya wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk akifunga kikao cha viongozi wa EU amesema Urusi na vitendo vyake ni tatizo kubwa la kimkakati linaloikabili Ulaya.

Akiongoza kikao cha wakuu wa nch ishirini na nane za Umoja wa Ulaya. Bw. Tusk amesema kuwa vitendo vya Urusi ndani ya Ukraine na katika Ulaya ni changamoto na alibaini kwamba mataifa ya Umoja wa Ulaya yameungana zaidi kuliko ilivyowahi kuwa huko nyuma katika kukabiliana na Urusi.

Aidha, ameonya kuwa Ulaya inahitaji mkakati wa muda mrefu wa aina yake,ambao si tu utakaoshughulikia matatizo katika wiki zijazo na miezi, bali miaka. Wakati huo huo viongozi wamekubaliana vikwazo vipya vinavyopiga marufuku uwekezaji katika jimbo la Crimea, ishara kwamba vikwazo hivyo havitalegezwa hadi Urusi itakapobadili msimamo wake kuhusu jimbo hilo.
Source: BBC

Thursday, December 18, 2014

MANENO YA MAMA TIBAIJUKA KATIKA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA ESCROW.



 “Mimi Nijiuzulu kwa sababu gani? yaani kwa sababu ya mafanikio ya kuwakomboa wanawake kwenye Elimu ndio mimi nijuzulu,maana kujiuzulu kunasababu, na hakuna sababu ya mimi kufanya hivyo na sitofanya hivyo kwani wanaodai mimi nijiuzulu ni wanafiki wenye nia mbaya na mimi ,na mimi sijiuzulu ng’o na nikifanya wanavyotaka Rais atashangaa ”alisema Waziri Tibaijuka.

“Leo natuhumiwa na kila mtu kwamba nimepewa pesa na Rugimalira kwamba ni za kifisadi,Jamani tuwe wa kweli kuhusu madai haya maana nimepewa pesa na Rugemalira kwa ajiri ya shule hizi na sio huyo pekee alliyechangia kwani waliochangia pesa hizi ni watu wengi ikiwema Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Mfanya Biashara Maarufu Reginald Mengi na wengine wengi,inakuwaje leo mchango wa Rugumarila kwa Ajiri ya Elimu kwenye Shule hii ndio iwe nongwa”

“Kwasababu ukisema ni pesa alizonipa ni za ufisadi wa Escrow sio kweli,kwani Bodi ya Shule ilimuomba Bwana Rugemalira pesa kwa kutumia Kampuni yake ya Mabibo Wine na kipindi kile ndio alikuwa kiongozi, sasa hawa watu wanaozani ni za ufisadi inakuwaje jamani tuwe wakweli”Aliongeza Waziri Tibaijuka."
Source: Clouds fm radio

Rihanna aajiriwa na Puma


Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna anajiandaa kuanza kufanya kazi katika kampuni ya michezo Puma.Mwanamziki huyo ametangazwa kuwa mkurugenzi wa ubunifu wa vifaa vya kike na atakuwa uso wa vifaa vya mazoezi vya wanawake.
Rihana mwenye umri wa miaka 26 ataunda aina ya nguo zilizopo pamoja na viatu na kusaidia kubuni muundo mpya wa chapa cha bidhaa hizo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo,Rihana amesema anafurahi kuona ni nini yeye na Puma wanaweza kubuni.

Wakuu wa kampuni ya Puma wanasema kuwa Rihana ataleta ubunifu katika ulimwengu wa riadha.
Nguo hizo mpya zitakuwa na mtindo wenye lengo la kuwaimarisha wanawake katika mazoezi mbali na kuwafanya kuamini miili yao pamoja na wao wenyewe. Jukumu la Rihana litakuwa kuwa na ushawishi katika bidhaa zitakazoundwa pamoja na kuandaa ukuzaji wa bidhaa mpya. Akiwa miongoni mwa kampeni ya Forever faster msanii huyo atashirikishwa na wanariadha kama viule Usain Bolt na Sergio Aguero.

 
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bjorn Gulden amesema kuwa waliamua kumtafuta mshirika katika nguo za wanawake za kufanyia mazoezi kutokana na ushawishi mkubwa wa kampuni hiyo katika soka,riadha na mashindano ya magari.Tunafurahi kumpata Rihana na tunajianda kuona ni nini tunaweza buni kwa ushirikiano wake.

Rihana si mtu wa kwanza nje ya michezo kujiunga na kampuni ya Puma. Msanii 50 cent na Jay Z walitoa viatu na kampuni ya Reebok, huku Kim Kardashian akiwa uso wa viatu vya Sketchers na mumewe Kanye West akifanya kazi na Nike pamoja na Adidas.

Wabunge warushiana ngumi bungeni Kenya


Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
 
 Seneta Johnston Muthama alijikuta pabaya kwani suruali yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.


 
Seneta Muthama pia alijeruhiwa vibaya mguuni

Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.

Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia.

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Source: BBC

Kombe la Dunia kuchezwa Mei na June?




Chama cha vilabu vikubwa vya soka barani ulaya (ECA) wanataka michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022 yatayofanyika nchi Qatar yafanyike kati ya Mei 5 na Juni 4. 
 
Shirikisho la soka duniani Fifa walitangaza mwezi uliopita kuwa michezo ya michuano hiyo itafanyika kati ya Januari na Februari au Novemba na desemba.  Lakini mapendekezo yanayotolewa na Chama cha vilabu vikubwa vya soka (ECA) na wakilishi wa ligi za kulipwa ulaya (EPFL) wanataka mashindano hayo yacheze mwanzo mwa majira ya joto sababu itakua ndio salama kwa afya za wachezaji.
 
Uamuzi wa shirikisho la mpira dunia Fifa kuhusu wakati gani michuano hiyo ifanyike inatarajiwa kutolewa Machi mwaka 2015. ECA na EPF wanaamini pendekezo yao mpya yanaonyesha jinsi mashindano inaweza kuchezwa Mei na Juni bila kuhatarisha afya za wachezaji na viongozi.

 Pia kufanyika kwa kombe la dunia mwezi mei na juni kutakua hakuna madhara kwa michuano ya klabu bigwa barani ulaya, michezo ya olimpiki na waumini wa dini ya kiislam watakua wamemaliza mfungo mtukufu wa Ramadhani 

.Source: Mjengwa

Wednesday, December 17, 2014

Diamond akwea pipa aenda Uganda kwenye ''White Paty'' ya Zari

Staa wa Bongo Fleva,Diamond Platinumz amekwea pipa leo kuelekea nchini Uganda kwenye ''''White Paty'' inayoandaliwa na anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa sasa aishiye nchini humo. Zari.Kupitia mtandao wa Instagram Diamond aliandika hivi.....KAMPALA!!! UGANDA!!! your boy is on his way... #Zari_AllWhite_CirocParty.
Zari The boss lady.
Source: Clouds fm

Hii taarifa inawahusu wale watoto wawili wa Tanzania waliokua wameungana vifua.



Watoto 1Bila shaka kila aliekua anawafatilia au kusikia taarifa za hawa watoto atakua na hamu ya kujua kimeendelea nini baada ya kupelekwa kutibiwa nchini India ambapo mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amethibitisha kupitia ukurasa wake wa twitter kwa kuyaandika haya.
Hospitali ya Apollo lndia imefanikiwa kuwatenganisha watoto mapacha toka Tanzania waliokuwa wameungana vifua‘
Source: Millard Ayo

NAPE APONGEZA WAPINZANI

NapeNnauye_480_280_2238a.jpg

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimevipongeza vyama vingine vya siasa nchini kwa ushiriki wao kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwataka waongeze kasi kwani ushindi wao wa asilimia 14 hadi sasa ni mdogo, ukilinganisha na umri wa mfumo wa vyama vingi nchini ambao ni miaka 20.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye alisema vyama vya upinzani vinapaswa kupongezwa kwa kushiriki kwenye uchaguzi huo na kwamba kwa maeneo waliyoshinda wanapaswa kuwaletea maendeleo wananchi, ili wasipoteze imani kwao.

Alisema pamoja na ushindi huo, vyama hivyo visitarajie mabadiliko makubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani wa madiwani, wabunge na Rais, kwani pamoja na kupata asilimia hizo 14, hali haitabadilika ukilinganisha na ushindi wa CCM.

“Ni kweli pamoja na kwamba uchaguzi kama huu uliopita CCM ilishinda kwa asilimia 96 na mwaka huu kwa asilimia 84, bado sio kigezo cha vyama vya upinzani kufanya vizuri zaidi ya asilimia hizo 14 walizoambulia hadi sasa kwa maeneo ambayo matokeo yametoka”, alisema Nape.

Alisema hata maeneo ambayo uchaguzi utarudiwa, sio rahisi vyama hivyo kupata ushindi wa kishindo, kwani hadi sasa wameshaona mwelekeo wa kukubalika kwao kwa wananchi.
Alisema kwa matokeo hayo, vyama vya upinzani zinapaswa kuongeza kasi kwani tangu mfumo wa vyama vingi uanze kutumika nchini ni miaka 20 sasa na bado vyama hivyo havijakua ipasavyo. 
Source: Mjengwa blog

Wednesday, December 3, 2014

RUSHWA SI AFRIKA PEKEE , NI UGONJWA UNAOSUMBUA SASA HATA NCHI ZILIZOENDELEA

Transparency International yasema rushwa ni tatizo kwa wote

Riport na DW

Katika ripoti yake ya leo (03.12.2014) shirika hilo lilisema rushwa inaonekana kukithiri Uturuki na China na limetaka kuwepo ushirikiano wa karibu wa kimataifa kuangamiza kabisa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Katika ripoti yake shirika la Transparency International hilo lenye makao yake Berlin Ujerumani lilisema rushwa ni tatizo kwa uchumi na kuna umuhimu wa taasisi kubwa za fedha katika Umoja wa Ulaya na Marekani kufanya kazi pamoja na nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kuwakomesha mafisadi wasikwepe mkono wa sheria.

Katika faharasa ya 20 inayoonyesha viwango vya rushwa katika mataifa 175, China imepata alama 36 kati ya 100, Uturuki imepata 45 na Angola 19, zikiwa nchi ambazo zimeanguka kwa alama kati ya 4 na 5, licha ya uchumi wao kukua kwa wastani wa asilimia 4 katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Transparency International hutoa alama 100 kwa nchi ambayo haina visa vya rushwa na sufuri kwa nchi ambayo rushwa imeshamiri.

Kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda imefanya vyema katika kupambana na rushwa ikishikilia nafasi ya 55, ikifuatiwa na Tanzania katika nafasi ya 119, na Uganda ni ya tatu katika nafasi ya 142. Kenya ni ya nne katika nafasi ya 145 na Burundi inashika mkia katika jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 159.

Zaidi ya theluthi mbili kati ya nchi 175 katika faharasa hiyo zimepata pointi chini ya 50 huku Somalia, Korea Kaskazini, Sudan, Afghansitan na Sudan Kusini kwa mara nyingine tena zikishika nafasi za chini.

Mkurugenzi wa Transparency International katika mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara, Chantal Uwimana, alisema, "Vipindi vya mizozo huchochea rushwa, kuyumba kwa hali ya kisiasa na kukosekana uthabiti kwa sababu mifumo hudhoofika au wale wanaotakiwa kuisimamia mifumo hii wanapoteza muelekeo.Si jambo la kushangaza kwamba Sudan Kusini na Somalia ambazo zimekabiliwa na vita kwa muda mrefu zinaonekana kuwa na vitendo vya rushwa iliyokithiri."

Denmark ni mfano wa kuigwa

 Nchi iliyofanya vizuri kabisa na kushika nafasfi ya kwanza ni Denmark ikijipatia pointi 92, ikifuatiwa na New Zealand, Finland, Sweden na Norway, zote kwa mara nyingine tena zikiwa katika tabaka la nchi tano za kwanza aktika faharasa ya rushwa.
Infografik Korruptionsindex 2014 Englisch  
Faharasa kuhusu rushwa ya mwaka 2014

Ukraine ilipata pointi 26 na kubakia kuwa nchi inayoongoza kwa kiwango kikubwa cha rushwa barani Ulaya. Italia,Ugiriki na Romania kwa pamoja zimafanya vibaya miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zikiwa na pointi 43.

Mwenyekiti wa Transparency International, José Ugaz alisema maafisa mafisadi huficha mali walizozipata kwa njia isiyo halali na kuzificha katika maeneo salama kupitia kampuni. Ugaz aidha amesema ufisadi mkubwa katika nchi zenye uchumi mkubwa haukandamizi tu haki za binadamu kwa watu masikini, bali pia husababisha matatizo ya utawala na uthabiti.

Ripoti hiyo ilizitaka nchi zinazoshika mkia katika orodha iliyochapishwa zichukue hatua madhubuti za makusudi kupambana na rushwa kwa masilahi ya umma. Ugaz aliyataka mataifa yanayoshika nafasi za juu katika faharasa hiyo yasieneze vitendo vya ufisadi katika nchi ambazo hazijaendelea.
Shirika la Transparency International liliuhimiza Umoja wa Ulaya, Marekani na kundi la G20 la mataifa yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi, kuiga mfano wa Denmark na kuanzisha daftari la umma linalojumuisha tarifa muhimu za wamiliki kwa kampuni zote zilizoshirikishwa.

HUYU DIAMOND PLATNAMZ TAYARI AMEISHIKA AFRIKA HIVI HIVI KIUTANI UTANI


Post Ya Msanii AKA Kuhusu Mapokezi Ya Diamond Tanzania.

By 
Aka
AKA ni miongoni  mwa rappers wakali Africa ambaye hivi karibuni alikuwa South Africa na alishinda tuzo moja ya Channel O  ambako pia Diamond alikuwepo huko. Aka ame Repost video ya mapokezi ya Diamond iliyowekwa Sammisago.com na Kwenye Instagram ya Sammisago huku akiweka huu ujumbe.
Diamond lands back in Tanzania after winning 3 Channel O Awards and this happens … Imagine South Africans felt like this about their own artists … In my country this is something reserved for the Bieber’s and Breezy’s … Where is our pride? Where is our passion? Anyways … BIG UP DIAMOND.
aka 2 Aka